Mattayo MT. 26
26
1IKAWA Yesu alipomaliza maneno haya yote, akawaambia wanafunzi wake, 2Mwajua ya kuwa baada ya siku mbili itakuwa pasaka, na Mwana wa Adamu atasalitiwa apate kusulibiwa. 3Ndipo makubani wakuu, na waandishi, na wazee wa watu wakakusanyika katika behewa ya kuhani mkuu aliyeitwa Kayafa; 4wakafanya shauri pamoja, illi wamkamate Yesu kwa hila na kumwua. 5Wakanena, Sio wakati wa siku kuu, isije ikatokea ghasia katika watu.
6Nae Yesu, alipokuwa Bethania katika nyumba ya Simon mwenye ukoma, 7mwanamke mwenye chombo cha alabastro cha marhamu ya thamani kubwa alimkaribia, akaimimina kichwani pake alipoketi akila. 8Wanafunzi wake walipoona, wakachukiwa, wakinena, Ya nini upotevu huu? 9Maana marhamu hii ingaliweza kuuzwa kwa fedha nyingi wakapewa maskini. 10Yesu akijua akawaambia, Mbona mnamtaabisha mwanamke? Maana ni kazi njema aliyonitendea mimi. 11Kwa maana siku zote maskini mnao pamoja nanyi; lakini mimi hamnami siku zote. 12Maana kwa kunimwagia mwili wangu marhamu hii, ametenda hivi illi kuniweka tayari kwa maziko yangu.
13Amin, nawaambieni, Killa ikhuhiriwapo injili hii katika ulimwengu wote, na hilo alilolitenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake.
14Kisha mmoja wa wale thenashara, jina lake Yuda Iskariote, alikwenda zake kwa makuhani wakuu, 15akasema, Nini mtakayonipa, nami nitamsaliti kwenu? Wakampimia vijiande thelathini vya fedha. 16Tokea wakati huo akawa akitafuta nafasi ajiate kumsaliti.
17Hatta siku ya kwanza ya mikate isiyotiwa chachu, wanafunzi wake wakamwendea Yesu, wakamwambia, Wapi unataka tukuandalie uile pasaka? 18Akasema, Enendeni mjini kwa mtu fulani, mkamwambie, Mwalimu anena, Majira yaugu i karibu; kwako nitafanya pasaka pamoja na wanafunzi wangu. 19Wanafunzi wakatenda kama Yesu alivyowaagiza, wakaiandaa pasaka. 20Bassi ilipokuwa jioni akaketi chakulani pamoja na wale thenashara. 21Walipokuwa wakila, akasema, Amin, nawaambieni, Mmoja wenu atanisaliti. 22Wakahuzunika sana, wakaanza kumwambia mmoja mmoja, Ni mimi, Bwana? 23Akajibu, akasema, Yeye aliyetia mkono wake pamoja nami katika sahani, ndiye atakaenisaliti. 24Mwana wa Adamu aenda zake, kama alivyoandikiwa: lakini ole wake mtu yule ambae Mwana wa Adamu anasalitiwa nae! Ingekuwa kheri kwake mtu yule kama asingalizaliwa. 25Yuda, yule mwenye kumsaliti, akajibu, akasema, Ni mimi, Rabbi? Akamwambia, Wewe umesema.
26Walipokuwa wakila, Yesu akatwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, Twaeni, mle; huu ni mwili wangu. 27Akatwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akinena, Nyweeni nyote hiki; 28maana hii ni damu yangu ya agano jipya, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. 29Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu leo nzao huu wa mzabibu, hatta siku ile nitakapounywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.
30Walipokwisha kuimba, wakatoka nje kwenda mlima wa Mizeituni. 31Yesu akawaambia, Ninyi nyote mtachukizwa kwa ajili yangu usiku huu: kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchunga, na kondoo wa kundi watatawanyika. 32Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitatangulia mbele yenu kwenda Galilaya. 33Petro akajibu, akamwambia, Wajapochukizwa wote kwa ajili yako, mimi sitachukizwa kabisa. 34Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, usiku huu kabla ya kuwika jogoo, utanikana marra tatu. 35Petro akamwambia, Ijaponipasa kufa nawe, sitakukana. Na wanafuuzi wote wakasema vivi hivi.
36Kiisha Yesu akaenda pamoja nao hatta kiwanja kiitwacho Gethsemane, akawaambia wanafunzi wake, Ketini hapa, hatta niende kule nikasali. 37Akamchukua Petro na wana wawili wa Zebedayo, akaanza kufadhaika, na kuhuzunika moyo. 38Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkakeshe pamoja nami.
39Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akiomba, akinena, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kinipitie; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe. 40Kisha akawaendea wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! hamkuweza kukesha pamoja nami hatta saa moja? 41Kesheni, kaombeni, msije mkaingia majaribuni: Roho ina nia njema, bali mwili ni dhaifu.
42Akaenda tena marra ya pili, akaomba, akinena, Baba yangu, ikiwa haiwezekani kikombe hiki kinipitie nisipokinywa, bassi, mapenzi yako yafanyike. 43Akaenda, akawakuta wamelala tena; maana macho yao yalikuwa mazito. 44Akawaacha tena, akaenda akaomba marra ya tatu, akisema maneno yaleyale. 45Khalafu akawaendea wanafunzi wake, akawaambia, Laleni sasa hatta mwisho, kapumzikeni: saa imekaribia, na Mwana wa Adamu anatiwa katika mikono ya wenye dbambi. 46Ondokeni, twende zetu. Angalieni, anaenisaliti anakaribia.
47Hatta alipokuwa akisema, Yuda, mmoja wa wale thenashara akaja, na pamoja nae makutano mengi, wana panga na marungu, wametoka kwa makuhani wakuu na wazee wa watu. 48Na yeye anaemsaliti amewapa ishara, akinena, Nitakaembusu, ndiye; mkamateni. 49Marra akamwendea Yesu, akasema, Salam, Rabbi, akambusu sana. 50Yesu akamwambia, Rafiki, umejia nini? Wakaenda, wakanyosha mikono yao wakamkamata Yesu. 51Mmoja wao waliokuwa pamoja na Yesu akanyosha mkono wake, akaufuta upanga wake, akampiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio. 52Yesu akamwambia, Rudisha upanga wako mahali pake: maana wote washikao upanga, wataangamia kwa upanga. 53Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu sasa hivi, akaniletea zaidi ya majeshi thenashara ya malaika? 54Yatatimizwaje bassi maandiko, kwamba hivyo ndivyo vilivyopasa kuwa?
55Saa ile Yesu akawaambia makutano, Je, mmetoka, mfano wa watu wafukuzao mnyangʼanyi mna panga na marungu, kunitwaa? Killa siku naliketi mbele zenu hekaluni, nikifundisha, wala hamkunikamata. 56Lakini jambo hili lote limekuwa, illi maandiko ya manabii yatimizwe. Ndipo wanafunzi wake wote wakamwacha, wakakimbia.
57Nao waliomkamata Yesu wakampeleka kwa Kayafa kuhani mkuu, walipokuwapo waandishi na wazee wamekusanyika. 58Na Petro akamfuata kwa mbali hatta behewa ya kuhani mkuu, akaingia ndani, akaketi pamoja na watumishi, auone mwisho. 59Makuhani wakuu na baraza yote wakatafuta ushuhuda wa nwongo juu ya Yesu, wapate kumwua; 60wasipate; na ijapokuwa walitokea mashahidi wa uwongo wengi, hawakupata. 61Baadae mashahidi wa uwongo wawili wakatokea wakasema, Huyu alisema, Naweza kulivunja hekalu ya Mungu, na kuijenga kwa siku tatu. 62Kuhani mkuu akasimama akamwambia, Hujibu neno? Hawa wanakushuhudiani? 63Lakini Yesu akanyamaza. Kuhani mkuu akamjihu, akamwambia, Nakuapisha Mungu aliye hayi, utuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu. 64Yesu akamwambia. Wewe umesema: lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwoua Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu. 65Marra kuhani mkuu akararua mavazi yake, akisema, Amekufuru: tuna haja gani ya mashahidi wengine? Sasa mmesikia kufuru yake: 66mwaonaje? Wakajibu, wakasema, Ana sharti ya kufa. 67Ndipo wakamtemea mate va uso, wakampiga konde; wengine wakampiga makofi, 68wakinena, Ee Kristo, ni nani aliyekupiga?
69Na Petro alikuwa ameketi nje behewani: kijakazi kimoja akamwendea, akanena, Wewe nawe ulikuwa pamoja na Yesu wa Galilaya. 70Akakana mbele ya wote, akinena, Sijui unenalo. 71Alipotoka nje hatta ukumbini, mwanamke mwingine akamwona, akawaambia watu waliokuwa huko, Na huyu nae alikuwa pamoja na Yesu Mnazareti. 72Akakana tena kwa kiapo, Simjui mtu huyu. 73Punde kidogo, wale waliosimama karibu wakamwendea, wakamwambia Petro, Hakika na wewe u mmoja wao; maana hatta usemi wako wakutambulisha. 74Ndipo akaanza kulaani na kuapa, Simjui mtu huyu. Marra akawika jogoo. 75Petro akalikumbuka lile neno la Yesu aliloambiwa nae, Kabla ya kuwika jogoo, utanikana marra tatu. Akatoka nje, akalia kwa majonzi.
Iliyochaguliwa sasa
Mattayo MT. 26: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

: