Mattayo MT. 28
28
1SABATO ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, akaenda Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, kulitazama kaburi. 2Na kumbe! palikuwa na tetemeko kubwa la inchi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka mbinguni, akakaribia akalifingirisha lile jiwe mbali ya mlango, akaketi juu yake. 3Na sura yake ilikuwa kama umeme, na mavazi yake meupe kama thuluji. 4Na kwa kumwogopa walinzi wakatetemeka, wakawa kama wafu. 5Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnanitafuta Yesu aliyesulibiwa. 6Hayupo hapa; kwa maana amefufuka kama alivyosema. Njoni, patazameni mahali alipolazwa Bwana. 7Shikeni njia upesi, kawaambieni wanafunzi wake, Amefufuka katika wafu; Tazama, anatangulia mbele yenu kwenda Galilaya; huko mtamwona: haya, nimewaambieni. 8Wakaondoka upesi kutoka kaburini, kwa khofu na furaha nyingi, wakaenda mbio kuwapasha wanafunzi wake khabari. 9Nao walipokuwa wakienda kuwapasha wanafunzi wake khabari, Yesu akakutana nao, akinena, Salam! Wakakaribia wakamshika miguu, wakamsujudia. 10Yesu akawaambia, Msiogope: enendeni, mkawaambie ndugu zangu waemle Galilaya, ndiko watakakoniona.
11Nao walipokuwa wakienda njiani, baadhi ya askari waliingia mjini, wakawapasha makuhani wakuu khabari za mambo yote yaliyotendeka. 12Wakakusanyika pamoja na wazee, wakafanya shauri, wakawapa askari fedha nyingi, 13wakinena, Semeni, ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala. 14Na jambo hili likisikilikana kwa liwali, tutasema nae, nanyi tutawaondoa shaka. 15Bassi wakazitwaa zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Na neno lile likaenea katika Wayahudi hatta leo.
16Na wale wanafunzi edashara wakaenda Galilaya hatta mlima ule aliowaagiza Yesu. 17Nao walipomwona, wakamsujudia; lakini wengine waliona shaka. 18Yesu akaja kwao, akasema nao, akinena, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na juu ya dunia. 19Bassi, enendeni, kawafanyeni mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 20mkiwafundisha kushika yote niliyowaamuru ninyi: nti tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hatta mwisho wa dunia. Amin.
Iliyochaguliwa sasa
Mattayo MT. 28: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

: