Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Mose 17

17
Aburamu anaitwa Aburahamu.
1Aburamu alipokuwa mwenye miaka 99, Bwana akamtokea Aburamu, akamwambia: Mimi ni Mungu Mwenyezi, uendelee machoni pangu na kunicha!#1 Mose 35:11; 2 Mose 6:3; 1 Mose 48:15. 2Hivyo tutaagana sote wawili, mimi na wewe, nami nitakufanya kuwa watu wengi sanasana. 3Ndipo, Aburamu alipomwangukia usoni pake, naye Mungu akaendelea kusema naye kwamba: 4Tazama! Nina agano na wewe, uwe baba yao mataifa mazima ya watu. 5Kwa hiyo usiitwe tena jina lako Aburamu (Baba mtukufu), ila jina lako liwe Aburahamu (Baba yao wengi)! Kwani nimekuweka kuwa baba yao mataifa mengi ya watu.#Rom. 4:11,17. 6Nitakupa wazao wengi sanasana, nikufanye kuwa mataifa, nao wafalme watatoka kwako. 7Nitalisimamisha agano langu, tuliloliagana mimi na wewe nao wa uzao wako wajao nyuma yako, liwe agano la vizazi vya kale na kale, niwe Mungu wako na Mungu wao wa uzao wako wajao nyuma yako.#1 Mose 12:2; 15:4-6. 8Nitakupa wewe nao wa uzao wako wajao nyuma yako nchi hii, unayoikaa ugeni, ndiyo nchi yote ya Kanaani, mwichukue, iwe yenu kale na kale, nami nitakuwa Mungu wao.#1 Mose 23:4; 35:27; Ebr. 11:9-16.
Agano la kutahiri.
9Kisha Mungu akamwambia Aburahamu: Liangalieni Agano langu, wewe nao wa uzao wako wajao nyuma yako, vizazi kwa vizazi! 10Nalo hili ndilo Agano langu la kuliangalia, tunaloliagana mimi na wewe nao wa uzao wako wajao nyuma yako: Kwenu sharti atahiriwe kila aliye wa kiume.#3 Mose 12:3; Tume. 7:8. 11Mkizikata nyama za magovi yenu, hii itakuwa kielekezo cha Agano, tuliloliagana mimi nanyi. 12Kwenu kila mtoto wa kiume aliye wa vizazi vyenu akimaliza siku nane sharti atahiriwe. Vivyo hivyo nao wazalia wa nyumbani nao wasio wa uzao wako walionunuliwa kwa fedha kwa wageni wo wote. 13Hao wazaliwa nyumbani mwako nao walionunuliwa kwa fedha zako sharti nao watahiriwe. Hili Agano langu la kuzikata hizo nyama za miili yenu sharti liwe la kale na kale. 14Kwa hiyo mtu mume mwenye govi asiyekatwa nyama ya govi lake sharti roho yake yeye ing'olewe, atoweke kwao walio wa ukoo wake, maana ni mwenye kulivunja Agano langu.
Sarai anaitwa Sara.
15Kisha Mungu akamwambia Aburahamu: Mkeo Sarai asiitwe tena jina lake Sarai, ila jina lake liwe Sara (Mama mkuu)! 16Kwani nitambariki, nikupatie kwake mtoto mume; nitakapombariki, atakuwa mama wa mataifa mazima, nao wafalme wa makabila ya watu watatoka kwake. 17Ndipo, Aburahamu alipomwangukia usoni pake, akacheka na kusema moyoni mwake: Itawezekanaje, mwenye miaka mia azaliwe mtoto? Huyu Sara aliye mwenye miaka 90 atazaaje?#1 Mose 18:12; 21:6; Luk. 1:18. 18Kwa hiyo Aburahamu akamwambia Mungu: Afadhali Isimaeli angepata kuwapo machoni pako!
Kiagio cha kuzaliwa kwake Isaka.
19Ndipo, Mungu aliposema: Ni kweli, mkeo Sara atakuzalia mtoto mume, nalo jina lake uliite Isaka (Acheka); naye ndiye, nitakayemsimamishia Agano langu kuwa la kale na kale kwao wa uzao wake wajao nyuma yake.#1 Mose 26:3. 20Hata kwa ajili ya Isimaeli nimekusikia: Tazama, nitambariki naye na kumpa wazao wengi na kumfanya kuwa wengi sanasana, atazaa wakuu 12, nami nitamfanya kuwa taifa kubwa. 21Lakini lile Agano langu nitamsimamishia Isaka, Sara atakayekuzalia siku zizi hizi za mwaka ujao. 22Mungu alipokwisha kusema naye, akapaa juu na kutoka kwake Aburahamu.#1 Mose 35:13.
Aburahamu anajitahiri pamoja nao wote, alio nao.
23Kisha Aburahamu akamchukua mwanawe Isimaeli nao wazaliwa wote wa nyumbani mwake nao wote, aliowanunua kwa fedha zake, watu waume wote pia waliokuwamo nyumbani mwake Aburahamu, akawakata nyama za magovi yao siku iyo hiyo, kama Mungu alivyomwambia. 24Aburahamu alikuwa mwenye miaka 99 alipokatwa nyama ya govi lake. 25Naye mwanawe Isimaeli alikuwa mwenye miaka 13 alipokatwa nyama ya govi lake. 26Siku iyo hiyo moja Aburahamu na mwanawe isimaeli walitahiriwa. 27Nao waume wote wa nyumbani mwake, wazalia wa nyumbani nao, aliowanunua kwa fedha kwa watu wasio wa kabila lake, wote walitahiriwa pamoja naye.

Iliyochaguliwa sasa

1 Mose 17: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia