Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Mose 19

19
Ubaya wao Wasodomu.
1Ilipokuwa jioni, wale malaika wawili wakafika Sodomu, naye Loti alikuwa amekaa langoni huko Sodomu. Alipowaona Loti akainuka kuwaendea njiani, akawaangukia usoni chini,#1 Mose 18:22. 2akawaambia: Mabwana, njoni kufikia nyumbani mwa mtumwa wenu, mlale, mwioshe miguu yenu! Kesho mtaondoka na mapema kwenda zenu; lakini wakakataa wakisema: Tutalala nje. 3Ndipo, alipowahimiza sana, mpaka wakifikia kwake; walipoingia nyumbani mwake, akawatengenezea cha kunywa, akachoma mikate isiyochachwa, nao wakala. 4Walipokuwa hawajalala bado, watu wa ule mji wa Sodomu, vijana kwa wazee, watu wote waliotoka pande zote wakaja, wakaizunguka hiyo nyumba, 5wakamwita Loti, wakamwuliza: Wako wapi wale waume waliokuja kwako usiku huu? Walete, watutokee, tupate kuwajua! 6Loti akawatokea hapo pa kuingilia na kuufunga mlango nyuma yake, 7akasema: Ndugu zangu, msifanye mabaya! 8Tazameni! Ninao wanangu wa kike wawili wasiojua bado mtu mume, nitawatoa, niwape ninyi, mwafanyizie yaliyo mema machoni penu; lakini waume hao msiwafanyizie neno, kwani kwa sababu hii wmeingia kivulini mwa kipaa changu. 9Wakasema: Ondoka hapa! Tena wakaambiana: Ni mgeni peke yake kwetu, tena anataka kutuamua. Wakamsonga sana huyu Loti wakitaka kuukaribia mlango, wauvunje.#2 Petr. 2:7-8. 10Ndipo, wale watu walipoitoa mikono yao, wakamwingiza Loti kwao nyumbani, kisha wakaufunga mlango. 11Lakini wale watu waliokuwa nje hapo pa kuingia nyumbani wakawapofusha macho, wadogo kwa wakubwa, wakashindwa kupaona hapo pa kuingia nyumbani.#2 Fal. 6:18.
Loti anapona na wanawe.
12Kisha wale waume wakamwambia Loti: Kama unao ndugu, wakweo na wanao wa kiume na wa kike nao wo wote walio wako humu mjini, wachukue, utoke nao mahali hapa! 13Kwani sisi tutapaangamiza mahali hapa; kwani makelele yao ni makubwa masikioni mwake Bwana, kwa hiyo Bwana ametutuma, tupaangamize.#1 Mose 18:20. 14Loti alipotoka kusema na wakwewe waliowaoa wanawe wa kike, akawaambia: Inukeni, mtoke mahali hapa! Kwani Bwana ataungamiza mji huu. Lakini machoni pao wakwewe alikuwa kama mtu anayetaka kuwachekesha tu.#4 Mose 16:21. 15Kulipopambazuka, wale malaika wakamhimiza Loti kwamba: Ondoka! Mchukue mkeo nao wanao wawili wa kike, ulio nao, usiuawe nawe kwa ajili ya manza za mji huu! 16Alipozuzuika, wale waume wakawashika mikono, yeye na mkewe na wanawe, kwa huruma, Bwana alizowapatia, wakawatoa mjini na kuwapeleka nje. 17Walipokwisha kuwatoa na kuwapeleka nje, akasema: Iponye roho yako! Usitazame nyuma, wala usisimame huku bondeni mahali pawapo pote, ila kimbilia milimani, usiuawe!#Mat. 24:16. 18Loti akawaambia: Usiseme hivyo, Bwana wangu! 19Kwa kuwa mtumwa wako aliona upendeleo machoni pako, ukazizidisha huruma zako, ulizonifanyia, uiponye roho yangu! Tazama, sitaweza kukimbilia milimani kwa kwamba: Yale mabaya yatanipata, nami nitakufa. 20Tazama, huko karibu uko mji wa kuukimbilia, nao ni mdogo; acha, niukimbilie huo, kwa kuwa mdogo, niiponye roho yangu! 21Naye akamwambia: Basi, hata katika neno hili nitakuitikia, nisiufudikize nao mji huo, uliousema. 22Jihimize kuukimbilia! Kwani siwezi kufanya lo lote, mpaka ufike humo. Kwa hiyo wakaliita jina la mji huo Soari (Mdogo). 23Loti alipoingia Soari, jua lilikuwa linachomoza.#5 Mose 29:23; Sh. 11:6; Yos. 1:9-10; 13:19.
Mji wa Sodomu nao wa Gomora unaangamizwa.
24Ndipo, Bwana aliponyesha mvua ya moto uliochanganyika na mawe ya kiberitiberiti kwenye miji ya Sodomu na Gomora; mvua hii ilitoka kwake Bwana mbinguni.#Amo. 4:11; Luk. 17:29; 2 Petr. 2:6. 25Ndivyo, Mungu alivyoifudikiza hiyo miji nalo hilo bonde lote pamoja na watu waliokaa humo mijini nayo majani yote yaliyochipuka katika nchi ile.#Luk. 17:32. 26Naye mkewe Loti alipoyatazama ya nyuma akawa nguzo ya chumvi. 27Kesho yake Aburahamu akaamka na mapema kwenda pale, aliposimama mbele ya Bwana. 28Akachungulia upande wa Sodomu na Gomora na upande wa nchi zote za bonde hilo, mara akaona, moshi ulivyopanda kutoka chini kama moshi wa tanuru. 29Lakini hapo, Mungu alipoiangamiza miji ya lile bonde, Mungu alimkumbuka Aburahamu, amtoe Loti katika mafudikizo hayo na kumpeleka pengine alipoifudikiza hiyo miji, Loti alimokuwa na kukaa humo.
Ukosaji mbaya wa wana wa kike wa Loti.
30Kisha Loti akatoka Soari, akapanda milimani kukaa huko pamoja na wanawe wawili wa kike, kwani aliogopa kukaa mle Soari; kwa hiyo akakaa pangoni yeye pamoja na wanawe wawili. 31Kisha yule wa kwanza akamwambia mdogo wake: Baba yetu ni mzee, tena hakuna mtu mume katika nchi hii yote wa kuingia kwetu, kama ilivyo desturi po pote duniani. 32Haya! Na tumlevye baba yetu kwa mvinyo, kisha tulale naye, tupate kwa baba yetu mimba za kuukalisha mlango!#3 Mose 18:7. 33Basi, wakamlevya baba yao usiku huo, kisha yule mkubwa akaingia kwa baba yake, akalala naye, lakini mwenyewe hakujua, alipokuja kulala naye, wala alipoondoka. 34Kesho yake yule mkubwa akamwambia mdogo wake: Tazama, usiku wa jana nimelala na baba yangu; haya! Na tumlevye kwa mvinyo hata siku ya leo, upate kuingia kwake na kulala naye, tupate kwa baba yetu mimba za kuukalisha mlango! 35Kisha wakamlevya baba yao kwa mvinyo nao usiku huo, naye mdogo akaingia, akalala naye, lakini mwenyewe hakujua, alipokuja kulala naye, wala alipoondoka. 36Hivyo ndivyo, wana wa kike wa Loti wote wawili walivyopata mimba kwa baba yao. 37Yule mkubwa alipozaa mtoto mume akamwita jina lake Moabu (Wa baba), naye ni baba yao Wamoabu mpaka leo.#5 Mose 2:9. 38Yule mdogo alipozaa mtoto mume akamwita jina lake Ben-Ami (Mwana wa Kwetu), naye ni baba yao wana wa Amoni mpaka leo.#5 Mose 2:19.

Iliyochaguliwa sasa

1 Mose 19: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia