1 Mose 23
23
Kufa na kuzikwa kwake Sara.
1Siku zake Sara za kuwapo zilipopata miaka 127, hii miaka ya kuwapo kwake ilipotimia, 2Sara akafa huko Kiriati-Arba, ndio Heburoni, katika nchi ya Kanaani; ndipo, Aburahamu alipoingia nyumbani kumwombolezea na kumlilia.
3Kisha Aburahamu akaondoka kwa mfu wake, akasema na wana wa Hiti kwamba: 4Mimi ni mgeni anayejikalia tu kwenu, nipeni kwenu mahali pa kaburi, pawe pangu, nipate kumzika mfu wangu aliomo nyumbani kwangu! 5Nao wana wa Hiti wakamjibu Aburahamu kwamba: 6Tusikie, bwana wetu! Wewe u mkuu wa Mungu kwetu; mzike mfu wako katika kaburi lo lote la kwetu, utakalolichagua! Hakuna mtu wa kwetu atakayekunyima kaburi lake, kwamba usimzike mfu wako humo. 7Ndipo, Aburahamu alipoinuka, akawainamia watu wa nchi hii, wao wana wa Hiti, 8akasema nao kwamba: Roho zenu zikiitikia kwamba: Nimzike mfu wangu aliomo nyumbani mwangu, nisikilizeni, mniombee kwa Efuroni, mwana wa Sohari, 9anipe lile pango lake la Makipela lililoko penye mwisho wa shamba lake! Akinipa, nitamlipa katikati yenu fedha zote pia za kulinunua, liwe mahali pangu mimi pa kuzikia. 10Naye Efuroni alikuwa amekaa papo hapo katikati ya wana wa Hiti; ndipo, huyu Mhiti Efuroni alipomjibu Aburahamu masikioni pao Wahiti wote waliokuja hapo langoni penye mji wake kwamba: 11Sivyo, bwana wangu. Nisikie! Hilo shamba ninakupa, nalo pango lililomo ninakupa, machoni pao hawa wana wa ukoo wangu ninakupa, upate kumzika mfu wako. 12Ndipo, Aburahamu alipowainamia tena watu wa nchi hii, 13akamwambia Efuroni masikioni pa watu wa nchi hii kwamba: Ungenisikia tu! Chukua kwangu hizi fedha za kulinunua shamba hilo, nitakazokupa, nipate kumzika mfu wangu huko! 14Efuroni akamjibu Aburahamu kwamba: 15Bwana wangu, nisikie tu! Shamba la fedha 400 ni kitu gani, tubishane mimi na wewe? Mzike tu mfu wako! 16Aburahamu akamwitikia Efuroni; kwa hiyo Aburahamu akampimia Efuroni hizo fedha, alizozisema masikioni pao wana wa Hiti, fedha 400, wachuuzi walizozitumia, ndio shilingi 1600. 17Basi, shamba la Efuroni lililokuwa huko Makipela mbele ya Mamure, hilo shamba lenyewe pamoja na lile pango lililokuwako, nayo miti yote ya hapo shambani iliyokuwako mipakani katika mipaka yake ya pande zote, 18yote pamoja yakawa mali yake Aburahamu machoni pao wana wa Hiti wote waliokuja langoni penye mji wake.
19Baadaye Aburahamu akamzika mkewe Sara katika hilo pango la shamba la Makipela lililoko mbele ya Mamure, ndio Heburoni, katika nchi ya Kanaani. 20Ndivyo, hilo shamba pamoja na hilo pango lililoko lilivyotolewa kuwa mali yake Aburahamu, liwe mahali pake yeye pa kuzikia, likikoma kuwa lao wana wa Hiti.#1 Mose 25:9-10; 47:30; 49:29-30; 50:13.
Iliyochaguliwa sasa
1 Mose 23: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.

: