1 Mose 26
26
Isaka anabarikiwa na Bwana huko Gerari kwa Wafilisti.
1Njaa ikaingia katika nchi hiyo kuliko ile njaa ya kwanza iliyokuwako siku za Aburahamu; ndipo, Isaka alipokwenda Gerari kwa Abimeleki, mfalme wa Wafilisti.#1 Mose 12:10; 20:2. 2Ndiko, Bwana alikomtokea na kumwambia: Usitelemke kwenda Misri! Kaa katika nchi, nitakayokuambia! 3Kaa ugenini katika nchi hii, mimi nitakuwa pamoja na wewe, nikubariki. Kwani wewe nao wa uzao wako nitawapa nchi hizi zote, nikitimize kiapo, nilichomwapia baba yako Aburahamu.#1 Mose 12:7; 22:16. 4Nitawafanya wao wa uzao wako kuwa wengi kama nyota za mbinguni, nazo nchi hizi zote nitawapa wao wa uzao wako, namo katika uazo wako ndimo, mataifa yote ya nchini yatakamobarikiwa,#1 Mose 15:5; 12:3; 22:18. 5kwa kuwa Aburahamu aliisikia sauti yangu, akayaangalia maneno yangu yapasayo kuangaliwa: maagizo yangu na maongozi yangu na maonyo yangu.
Rebeka analindwa, asipatwe na mabaya kwake Abimeleki.
6Isaka alipokaa Gerari, 7nao waume wa mahalai hapo walipomwuliza habari ya mkewe, akasema: Huyu ni dada yangu, kwani aliogopa kusema: Ni mke wangu, kwa kwamba: Waume wa mahali hapa wasije kuniua kwa ajili ya Rebeka, kwani ni mzuri wa kumtazama. 8Alipokwisha kukaa huko siku nyingi, Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, akachungulia dirishani, akaona, Isaka alivyomchekesha mkewe.#Fano. 5:18. 9Ndipo, Abimeleki alipomwita Isaka, akasema: Kumbe huyo ni mkeo! Umewezaje kusema: Huyu ni dada yangu? Isaka akamwambia: Ni kwa kuwa nilisema: Nisiuawe kwa ajili yake! 10Abimeleki akasema: Kwa nini umetufanyizia hivyo? Hili lingekuwa jambo kubwa, mtu wa kwetu akilala na mkeo, nawe ungalitukosesha sana. 11Kwa hiyo Abimeleki akawatangazia watu wake wote kwamba: Atakayemgusa mtu huyu au mkewe hana budi kuuawa.
Mali zake nyingi zinampatia Isaka matata kwa Wafilisti.
12Isaka alipopanda mbegu katika nchi hiyo, akavuna mia mwaka huo, maana Bwana alimbariki.#Fano. 10:22. 13Akawa mtu mkuu, akaendelea vivyo hivyo kuwa mkuu, mpaka akiwa mkuu kabisa. 14Akawa na makundi ya mbuzi na kondoo, nayo makundi ya ng'ombe, nao watumwa wengi, kwa hiyo Wafilisti wakamwonea wivu; 15navyo visima vyote, watumwa wa baba yake walivyovichimbua siku za baba yake Aburahamu, Wafisiti walikuwa wameviziba na kuvijaza mchanga.#1 Mose 21:25. 16Naye Abimeleki akamwambia Isaka: Toka kwetu! Kwani umepata nguvu za kutushinda sisi kabisa. 17Basi, Isaka akatoka huko, akapiga kambi katika bonde la Gerari, akakaa huko. 18Ndipo, alipovirudia na kuvichimbua tena vile visima vya maji, walivyovichimbua siku zile za baba yake Aburahamu, Wafilisti walivyoviziba, Aburahamu alipokwisha kufa, akaviita majina yaleyale, baba yake aliyoviita. 19Namo mle bondeni, watumwa wa Isaka walipochimba maji, wakapata kisima chenye maji yarukayo. 20Lakini wachungaji wa Gerari wakagombana nao wachungaji wa Isaka kwamba: Maji ni yetu! Ndipo, alipokiita hicho kisima jina lake Eseki (Ukorofi), kwa kuwa walimkorofisha huko. 21Walipochimbua kisima kingine, wakagombana nao hata kwa ajili yake hicho, akakiita jina lake Sitina (Upingani). 22Kisha akayavunja mahema yake huko, akachimbua kisima kingine; kwa kuwa hawakugombana naye kwa ajili yake hicho, akakiita jina lake Rehoboti (Papana) akisema: Sasa Bwama ametupanulia, tupate kuenea katika nchi hii. 23Kisha akatoka huko kwenda kupanda Beri-Seba. 24Huko Bwana akamtokea usiku uleule, akamwambia: Mimi ni Mungu wa baba yako Aburahamu; usiogope! Kwani mimi niko pamoja na wewe, nikubariki na kuwafanya wao wa uzao wako kuwa wengi kwa ajili ya mtumishi wangu Aburahamu. 25Ndipo, Isaka alipojenga huko pa kutambikia, akalitambikia Jina la Bwana, akalipiga hema lake huko, nao watumwa wake Isaka wakachimbua huko kisima.#1 Mose 12:8.
26Huko Abimeleki na rafiki zake Ahuzati na Pikoli, mkuu wa vikosi, wakamwendea na kutoka Gerari.#1 Mose 21:22. 27Isaka akawauliza: Kwa nini mmekuja kwangu ninyi mnaonichukia, mkanifukuza kwenu? 28Wakasema: Tumeona kwa macho yetu, ya kuwa Bwana yuko pamoja na wewe, kwa hiyo tukasema: Na tufanye maagano na wewe na kuapiana sisi na wewe! 29Usitufanyie mabaya, kama sisi tusivyokugusa, kama sisi tulivyokufanyia mema tu, tukakuacha, uende zako na kutengemana. Nawe sasa umebarikiwa hivyo na Bwana. 30Ndipo, alipowafanyia karamu, wakala, wakanywa. 31Kesho yake wakaamka na mapema, wakaapiana kila mmoja na mwenziwe, kisha Isaka akawasindikiza, wakitoka kwake kwenda zao na kutengemana.
32Ikawa siku hiyo, wakaja watumwa wake Isaka kumpasha habari za kile kisima, walichokichimbua, wakamwambia: Tumeona maji. 33Naye akakiita jina lake Siba (Kiapo); kwa sababu hii mji huo unaitwa jina lake Beri-Seba (Kisima cha Kiapo) mpaka siku hii ya leo.#1 Mose 21:31.
Ndoa ya kwanza ya Esau.
34Esau alipokuwa mwenye miaka 40 akamwoa Yuditi, binti Mhiti Beri; kisha naye Basimati, binti Mhiti Eloni.#1 Mose 36:2-3. 35Wote wawili wakamtia Isaka naye Rebeka uchungu mwingi rohoni.
Iliyochaguliwa sasa
1 Mose 26: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.

: