1 Mose 33
33
Yakobo anaonana na Esau na kupatana naye.
1Yakobo alipoyainua macho yake, atazame, mara akamwona Esau, akija pamoja na watu 400; ndipo, alipowagawanya watoto akimpa kila mama wake, Lea na Raheli na wale vijakazi wawili.#1 Mose 32:7. 2Nao hao vijakazi na wana wao akawaweka mbele, akafuata Lea pamoja na wanawe, naye Raheli pamoja na Yosefu akawaweka nyuma. 3Naye mwenyewe akawatangulia, akajiangusha chini mara saba, mpaka amfikie mkubwa wake karibu. 4Ndipo, Esau alipomkibilia, akamkumbatia na kumwangukia shingoni, akamnonea, nao wote wawili wakalia machozi. 5Alipoyainua macho yake akawaona wale wanawake na watoto, akauliza: Hawa, ulio nao, ni wa nani? Akasema: Ndio watoto, Mungu aliompa mtumishi wako.#Sh. 127:3. 6Ndipo, wale vijakazi walipofika karibu pamoja na watoto wao na kumwangukia. 7Kisha Lea naye akafika karibu pamoja na watoto wake na kumwangukia, mwisho akaja Raheli pamoja na Yosefu na kumwangukia. 8Akauliza tena: Hicho kikosi chako chote, nilichokutana nacho, ni cha nini? Akasema: Ni kwamba, nijipatie upendeleo machoni pa bwana wangu.#1 Mose 32:13-20. 9Esau akasema: Mimi ninazo mali nyingi, ndugu yangu; yashike yaliyo yako! 10Lakini Yakobo akajibu: Sivyo! Kama nimeona upendeleo machoni pako, yachukue matunzo haya mkononi mwangu! Kwa kuwa nilipouona uso wako, ikawa, kama nimeuona uso wake Mungu, maana umenipokea na kupendezwa.#2 Sam. 14:17. 11Sasa ipokee hiyo mbaraka, uliyoletewa! Kwani Mungu amenigawia mengi, nipate yote pia, nitoshewe. Ndivyo, aliyombembeleza, mpaka akiyachukua.#1 Sam. 25:27; 30:26. 12Kisha akasema: Na tuondoke, twende zetu! Nami na nikutangulie. 13Lakini Yakobo akamwambia: Bwana wangu anajua, ya kuwa watoto hawa ni wachanga bado, tena ninao mbuzi na kondoo na ng'ombe wenye kunyonyesha, wao wakikimbizwa kwenda zaidi siku moja tu, kundi lote litakufa. 14Kwa hiyo bwana wangu na amtangulie mtumishi wake; mimi na nifuate poleple, kama hawa nyama, ninaowapeleka, wanavyoweza kwenda, hata nifike kwa bwana wangu huko Seiri. 15Ndipo, Esau aliposema: Nitakuachia watu wengine wa kwangu, nilio nao; lakini akasema: Wafanye nini? Inatosha, nikiona upendeleo machoni pa bwana wangu. 16Basi, Esau akarudi siku hiyohiyo na kuishika njia yake ya kwenda Seiri.
Yakobo anatua Sikemu.
17Yakobo akaondoka kwenda Sukoti, akajijengea nyumba huko, nayo makundi yake akayajengea vibanda; kwa hiyo mahali pale pakaitwa Sukoti (Vibanda).
18Yakobo aliporudi kutoka Mesopotamia akafika na kutengemana kwenye mji wa Sikemu ulioko katika nchi ya Kanaani, akapiga kambi mbele yake huo mji. 19Akakinunua kile kipande cha shamba, alikolipiga hema lake, kwa wana wa Hamori, babake Sikemu, kwa fedha mia.#Yos. 24:32. 20Kisha akajenga huko pa kutambikia, akapaita Mungu Mwenyewe wa Isiraeli.#1 Mose 12:7-8.
Iliyochaguliwa sasa
1 Mose 33: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.

: