Yohana 1
1
Neno.
1Hapo mwanzo palikuwapo Neno; hilo Neno lilikuwapo kwa Mungu, naye Mungu ndiye aliyekuwa Neno.#Yoh. 17:5; 1 Yoh. 1:1-2; Ufu. 19:13. 2Hilo lilikuwapo hapo mwanzo kwa Mungu.#Fano. 8:22. 3Vyote viliumbwa nalo, pasipo hilo hakuna hata kimoja kilichoumbwa.#Kol. 1:16-17; Ebr. 1:2. 4Mwake hilo ndimo, uzima ulimokuwa, nao uzima ulikuwa mwanga wa watu.#Yoh. 5:26. 5Mwanga huu humulika gizani, lakini giza haikuushika.#Yoh. 3:19.
6Palitokea mtu aliyetumwa na Mungu, jina lake Yohana. 7Huyo alijia kushuhudu, aushuhudie mwanga, wote wapate kuutegemea kwa ajili yake.#Yoh. 1:19; Mat. 3:1; Luk. 1:13-17,57-80. 8Mwenyewe hakuwa mwanga, alikuja tu, aushuhudie mwanga.#Yoh. 1:20. 9Ndio mwanga wa kweli unaomwangaza kila mtu, tena ndio uliokuwa ukija ulimwenguni.#Yoh. 8:12. 10Ulikuwamo ulimwenguni, nao ulimwengu uliumbwa nao, lakini ulimwengu haukuutambua.#Yoh. 1:3-5. 11Alipofika mwake, wao waliokuwa wake hawakumpokea. 12Lakini wo wote waliompokea aliwapa nguvu, wapate kuwa wana wa Mungu, ndio wale waliolitegemea Jina lake.#Gal. 3:26. 13Hao hawakuzaliwa na damu wala na pendo la mwili wa mtu wala na pendo la mwanamume, ila wamezaliwa na Mungu.#Yoh. 3:5-6. 14Neno lilipopata kuwa mtu, akatua kwetu, nasi tukauona utukufu wake, ni utukufu kama wa mwana aliyezaliwa wa pekee na baba yake, kwani alikuwa mwenye magawio na kweli yote.*#Yes. 7:14; 60:1; 2 Petr. 1:16-17.
15*Yohana akamshuhudia yeye na kupaza sauti akisema: Huyu ndiye, niliyemsema: Ajaye nyuma yangu alikuwa mbele yangu, kwani ni mtangulizi wangu.#Yoh. 1:27,30. 16Kwani katika mema yake yaliyo mengi sisi sote tumetwaa magawio kwa magawio.#Yoh. 3:34; Kol. 1:19-20. 17Kwani Maonyo tulipewa na Mose, lakini ugawiaji na ukweli umekuja na Yesu Kristo.#Rom. 10:4. 18Hakuna mtu aliyemwona Mungu hapo kale po pote, Mwana wa Mungu aliyezaliwa wa pekee, aliyeambatana na Baba, ndiye aliyetusimulia.*#Yoh. 6:46; Mat. 11:27; 1 Yoh. 4:12.
Ushahidi wa Yohana.
19*Huu ndio ushahidi wa Yohana, Wayuda walipotuma kwake toka Yerusalemu watambikaji na Walawi, wamwulize: Wewe ndiwe nani?#Luk. 3:15-16. 20Akaungama pasipo kukana, akaungama: Mimi siye Kristo.#5 Mose 18:15; Mal. 4:4; Mat. 17:10. 21Walipomwuliza: Sasa je? Ndiwe Elia? akasema: Mimi siye. Ndiwe mfumbuaji? akajibu: Hapana. 22Wakamwambia: Ndiwe nani? tupate kuwajibu waliotutuma; wajisemaje? 23Akasema: Ndimi sauti ya mtu apigaye mbiu nyikani: Inyosheni njia ya Bwana, kama alivyosema mfumbuaji Yesaya.#Yes. 40:3; Mat. 3:3; Mar. 1:3; Luk. 3:4. 24Nao waliotumwa walikuwa wa Mafariseo. 25Walipomwuliza wakimwambia: Mbona unabatiza, kama wewe siwe Kristo wala Elia wala mfumbuaji? 26Yohana akawajibu: Mimi nabatiza katika maji; lakini kati yenu amesimama, msiyemjua ninyi,#Mat. 3:11; Mar. 1:7-8. 27ndiye anayekuja nyuma yangu, nami sifai kumfungulia ukanda wa kiatu chake.#Yoh. 3:26. 28Haya yalikuwapo huko Betania, ng'ambo ya Yordani, Yohana alikokuwa akibatiza.*
Mwana kondoo wa Mungu.
29Kesho yake akamwona Yesu, akija kwake, akasema: Mtazameni mwana kondoo wa Mungu anayeyaondoa makosa ya ulimwengu!#Yoh. 1:36; Yes. 53:7. 30Huyu ndiye, niliyemsema mimi: Nyuma yangu anakuja mtu aliyekuwa mbele yangu, kwani ni mtangulizi wangu.#Yoh. 1:15,27. 31Hata mimi sikumjua; ila kusudi afunuliwe Waisiraeli, ndiyo niliyojia na kubatiza katika maji. 32Kisha Yohana akamshuhudia akisema: Nimemwona Roho, anavyoshuka toka mbinguni kama njiwa na kumkalia.#Mat. 3:16; Mar. 1:10; Luk. 3:22. 33Nami sikumjua, lakini aliyenituma kubatiza katika maji ndiye aliyeniambia: Utakayemwona, Roho akimshukia na kumkalia, huyo ndiye anayebatiza katika Roho takatifu.#Luk. 3:2. 34Nami nimemwona, nikamshuhudia: Huyu ndiye Mwana wa Mungu.
Wanafuanzi wa kwanza.
35*Kesho yake Yohana akasimama tena na wanafunzi wake wawili, 36akamtazama Yesu, akitembea, akasema: Mtazameni mwana kondoo wa Mungu!#Yoh. 1:29. 37Wale wanafunzi wake wawili waliposikia, akisema hivyo, wakamfuata Yesu. 38Yesu akageuka, akawatazama, wanavyomfuata, akawauliza: Mwatafuta nini? Nao walipomwuliza: Rabi (maana yake ni kwamba: Mfunzi mkuu), unakaa wapi? 39akawaambia: Njoni, mwone! Basi, wakaja, wakapaona, anapokaa, wakakaa kwake siku ile, ikawa kama saa kumi. 40Mmoja wao hao wawili walioyasikia maneno ya Yohana na kumfuata Yesu alikuwa Anderea, ndugu ya Simoni Petero. 41Huyu akaanza kumwona Simoni aliyekuwa ndugu yake mwenyewe, akamwambia: Tumemwona Masiya (maana yake ni Kristo).#1 Sam. 2:10; Sh. 2:2; Yes. 61:1; Tume. 10:38. 42Alipokwenda naye kwa Yesu, Yesu akamtazama, akasema: Wewe ndiwe Simoni, mwana wa Yohana, wewe utaitwa Kefa (maana yake: Petero - Mwamba).*#Mat. 16:18.
Filipo na Natanaeli.
43*Kesho yake Yesu alipotaka kutoka kwenda Galilea akamwona Filipo, akamwambia: Nifuata! 44Lakini Filipo alikuwa mtu wa Beti-Saida, ni mji wao Anderea na Petero. 45Filipo akamwona Natanaeli, akamwambia: Tumemwona, ambaye mambo yake aliyaandika Mose katika Maonyo, hata Wafumbuaji, ndiye Yesu, mwana wa Yosefu wa Nasareti.#5 Mose 18:18; Yes. 7:14; 53:2; Yer. 23:5; Ez. 34:23. 46Natanaeli alipomwambia: Je? Kiko chema kinachoweza kutoka Nasareti? Filipo akamwambia: Njoo, uone!#Yoh. 7:41. 47Yesu alipomwona Natanaeli, akija kwake, akasema na kumwelekea kwamba: Tazameni! Mwisiraeli wa kweli asiye na udanganyifu! 48Natanaeli alipomwuliza: Umenitambua tangu lini? Yesu akajibu, akamwambia: Filipo alipokuwa hajakuita bado, ulipokuwa chini ya mkuyu, hapo nimekuona. 49Ndipo, Natanaeli alipomjibu: Mfunzi mkuu, wewe ndiwe Mwana wa Mungu, wewe ndiwe mfalme wa Isiraeli.#Yoh. 6:69; 2 Sam. 7:14; Sh. 2:7; Yer. 23:5; Mat. 14:33; 16:16. 50Yesu akajibu, akamwambia: Unanitegemea, kwa sababu nimekuambia: Nimekuona chini ya mkuyu; utaona makubwa kuliko hayo. 51Kisha akamwambia: Kweli kweli nawaambiani: Mtaona, mbingu zitakavyokuwa zimefunuka, nao malaika wa Mungu wanavyopanda, tena wanavyomshukia Mwana wa mtu.*#1 Mose 28:12.
Iliyochaguliwa sasa
Yohana 1: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.

: