Yohana 6
6
Kulisha watu 5000.
(1-15: Mat. 14:13-21; Mar. 6:32-44; Luk. 9:10-17.)
1*Kisha Yesu akaondoka kwenda ng'ambo ya bahari ya Galilea iitwayo ya Tiberia. 2Kundi la watu wengi likamfuata, kwani waliviona vielekezo, alivyowafanyia wagonjwa. 3Yesu akapanda mlimani, akakaa huko pamoja na wanafunzi wake. 4Lakini Pasaka ilikuwa karibu, ndiyo sikukuu ya Wayuda.#Yoh. 2:13; 11:55. 5Yesu alipoyainua macho yake, akaona kundi la watu wengi wanaomjia, akamwambia Filipo: Tununue wapi mikate, hawa wapate kula? 6Hivyo alivisema, amjaribu; kwani mwenyewe alijua, alichotaka kukifanya. 7Filipo akamjibu: Mikate ya shilingi 200 haiwatoshi, kila mmoja apate kidogo tu. 8Mmoja wao wanafunzi wake Anderea, nduguye Simoni Petero, akamwambia: 9Hapa yupo mtoto mdogo, anayo mikate mitano ya mofa na visamaki viwili. Lakini hivyo vitawafaa nini watu walio wengi kama hawa? 10Yesu akasema: Wakalisheni watu! maana mahali pale palikuwa na majani mengi; waliokaa waume tu walikuwa kama 5000. 11Kisha Yesu akaitwaa ile mikate, akashukuru, akawagawia waliokaa; vile vile navyo visamaki, kama walivyotaka. 12Lakini waliposhiba, akawaambia wanafunzi wake: Yakusanyeni makombo yaliyosalia, pasipatikane kinachopotea! 13Wakayakusanya, wakajaza vikapu kumi na viwili makombo ya mikate ile mitano ya mofa yaliyowasalia waliokula.
14Watu walipokiona kielekezo hicho, alichokifanya, wakasema: Kweli huyu ndiye mfumbuaji atakayekuja ulimwenguni.#5 Mose 18:15. 15Yesu alipowatambua, ya kuwa wanataka kuja, wamshike kwa nguvu, wamfanye mfalme, akaondoka tena akaja mlimani yeye peke yake tu.#Yoh. 18:36.
Yesu baharini.
(16-21: Mat. 14:22-33; Mar. 6:45-52.)
16Lakini jua lilipokwisha kuchwa, wanafunzi wake wakatelemka kwenda baharini, 17wakaingia chomboni, wavuke kwenda Kapernaumu ng'ambo ya bahari. Giza ilipokwisha kuingia, Yesu alikuwa hajafika kwao bado. 18Namo baharini mkainuka mawimbi kwa upepo uliovuma na nguvu. 19Walipokwisha endelea mwendo wa nusu saa na kupita kidogo, wakamwona Yesu, anavyokwenda juu ya bahari na kukifikia chombo karibu, wakaogopa. 20Ndipo, alipowaambia: Ni miye, msiogope! 21Walipotaka kumwingiza chomboni, mara chombo kikawa ufukoni kwenye nchi, walikokwenda.
Mkate uliotoka mbinguni.
22Kesho yake kundi la watu waliosimama ng'ambo ya bahari waliona, ya kuwa hakuwako chombo kingine huko, ni kile kimoja tu. Nao walikuwa wameona, ya kuwa Yesu hakuingia chomboni pamoja na wanafunzi wake; waliona, wanafunzi wake walivyoondoka peke yao. 23Lakini vyombo vingine vilivyotoka Tiberia vikafika karibu ya mahali pale, walipokula mikate, Bwana akiiombea.#Yoh. 6:11.
24*Watu walipoona, ya kuwa Yesu hayuko, ya kuwa wanafunzi wake hawako nao, wakaingia katika vile vyombo, wakafika Kapernaumu, wamtafute Yesu. 25Walipomwona ng'ambo ya bahari wakamwuliza: Mfunzi mkuu, umefika lini hapa? 26Yesu akawajibu akisema: Kweli kweli nawaambiani: Hamnitafuti, kwa maana mmeona vielekezo, ila kwa maana mmeila ile mikate, mkashiba. 27Sumbukieni vyakula! Lakini vile vinavyoangamia sivyo, ni vile vinavyokaa, viwafikishe penye uzima wa kale na kale, navyo ndivyo, Mwana wa mtu atakavyowapani ninyi. Kwani huyu ndiye, Baba Mungu aliyemwagiza hivyo na kumtia muhuri.#Yoh. 4:14; 5:31-36. 28Walipomwuliza: Tufanyeje, tupate kuzisumbukia kazi za Mungu? 29Yesu akajibu, akawaambia: Hii ndiyo kazi ya Mungu, mkimtegemea yeye, aliyemtuma.*#1 Yoh. 3:23. 30Wakamwambia tena: Wewe unafanya kielekezo gani, tukione, tukutegemee? Wewe unasumbukia nini?#Yoh. 2:18. 31Baba zetu walikula Mana jangwani, kama ilivyoandikwa: Aliwapa mikate iliyotoka mbinguni, waile.#2 Mose 16:13-14; Sh. 78:24. 32Yesu akawaambia: Kweli kweli nawaambiani: Mose siye aliyewapa ninyi mikate iliyotoka mbinguni, ila Baba yangu ndiye anayewapa ninyi mkate wa kweli utokao mbinguni.#Yoh. 6:49. 33Kwani mkate wa Mungu ndio ule ushukao toka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima. 34Ndipo, walipomwambia: Bwana, tupe siku zote mkate huo! 35Yesu akawaambia: Mimi ndio mkate wa uzima; ajaye kwangu hataona njaa, naye anitegemeaye hataona kiu hata siku moja.#Yoh. 4:14; 6:48; 7:37. 36Lakini ndivyo, nilivyowaambia: Mmeniona, lakini hamnitegemei.#Yoh. 6:26,29. 37Wote, Baba anipao, ndio watakaokuja kwangu; naye ajaye kwangu sitamfukuza, ajiendee.#Yoh. 17:6-8; Mat. 11:28. 38Kwani sikushukia toka mbinguni kuyafanya mapenzi yangu mimi, ila mapenzi yake yeye aliyenituma.#Yoh. 4:34. 39Nayo mapenzi yake yeye aliyenituma ndiyo haya: wote, alionipa, nisiwapoteze hata mmoja wao, ila niwafufue siku ya mwisho.#Yoh. 5:29; 11:24. 40Kwani haya ndiyo mapenzi ya Baba yangu: kila anayemtazamia Mwana na kumtegemea apate uzima wa kale na kale, nami nitamfufua siku ya mwisho.#Yoh. 5:29; 11:24.
41Wayuda wakamnung'unikia, kwa sababu alisema: Mimi ndio mkate ulioshuka toka mbinguni, 42wakasema: Huyu siye Yesu, mwana wa Yosefu? Hatumjui baba yake na mama yake? Asemaje sasa: Nimeshuka toka mbinguni?#Luk. 4:22. 43Yesu akajibu, akawaambia: Msinung'unike ninyi kwa ninyi! 44Hakuna awezaye kuja kwangu, Baba aliyenituma asipomvuta, nami nitamfufua siku ya mwisho.#Yoh. 6:65. 45Katika Wafumbuaji yameandikwa ya kwamba: Wote watakuwa wamefundishwa na Mungu. Kila amsikiaye Baba na kujifunza kuja kwangu.#Yes. 54:13; Yer. 31:33-34. 46Sisemi: Yuko aliyemwona Baba, asipokuwa yule aliyetoka kwa Mungu; huyo ndiye aliyemwona Baba.#Yoh. 1:18.
47*Kweli kweli nawaambiani: Anitegemeaye anao uzima wa kale na kale.#Yoh. 3:16. 48Mimi ndio mkate wa uzima.#Yoh. 6:35. 49Baba zenu walikula Mana jangwani, kisha wakafa.#Yoh. 6:31-32; 1 Kor. 10:3,5. 50Huu ndio mkate ushukao toka mbinguni, kwamba: Mwenye kuula asife! 51Mimi ndio mkate wenye uzima ulioshuka toka mbinguni. Mtu atakayeula mkate huu atakuwa mzima pasipo mwisho. Nao mkate, nitakaowapa mimi, ndio mwili wangu utakaotolewa, ulimwengu upate uzima.#Ebr. 10:5,10.
Kuula mwili wa Mwana wa mtu.
52Wayuda wakabishana wao kwa wao wakisema: Huyu atawezaje kutupa mwili wake, tuule? 53Yesu akawaambia: Kweli kweli nawaambiani: Msipoula mwili wa Mwana wa mtu, tena msipoinywa damu yake, hamna uzima mwenu. 54Mwenye kuula mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa kale na kale, nami nitamfufua siku ya mwisho.#Yoh. 6:63. 55Kwani mwili wangu ni chakula cha kweli, nayo damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56Mwenye kuula mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa mwangu, nami mwake.#Yoh. 15:4; 1 Yoh. 3:24. 57Kama Baba Mwenye uzima alivyonituma, tena kama mimi nilivyo mzima kwa nguvu ya Baba, vivyo hivyo naye mwenye kunila atakuwa mzima kwa nguvu yangu.* 58Huo ndio mkate ulioshuka toka mbinguni, si kama ile, baba zenu waliyoila, wakafa. Mwenye kuula mkate huu atakuwa mzima pasipo mwisho. 59Maneno haya aliyasema akifundisha nyumbani mwa kuombea huko Kapernaumu.
Wengi wakwazwa.
60*Wengi waliokuwa wanafunzi wake walipoyasikia wakasema: Neno hili ni gumu. Yuko nani awezaye kulisikia? 61Lakini Yesu kwa kujua moyoni mwake, ya kuwa wanafunzi wake wanalinung'unikia hilo, akawaambia: Hili linawakwaza? 62Vitakuwaje, mkiona, Mwana wa mtu anavyopaa huko, alikokuwa kwanza?#Yoh. 3:13. 63Roho ndiyo inayotupatia uzima, mwili haufai kitu. Maneno, niliyowaambia, ndiyo ya Kiroho yenye uzima.#2 Kor. 3:6. 64Lakini kwenu wako wasionitegemea. Kwani tangu mwanzo Yesu aliwajua wasiomtegemea, naye atakayemchongea alimjua vilevile.#Yoh. 13:11. 65Akasema: Kwa hiyo nimewaambia: Hakuna awezaye kuja kwangu, asipokuwa amepewa na Baba yangu.#Yoh. 6:44.
Kuungama kwake Petero.
66Tokea hapo wengi waliokuwa wanafunzi wake wakarudi nyuma, wasifuatane tena naye. 67Yesu alipowauliza wale kumi na wawili: Nanyi mwataka kujiendea? 68ndipo, Simoni Petero alipomjibu: Bwana, tumwendee nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa kale na kale.#Yoh. 6:63. 69Nasi tumekutegemea, tukatambua, ya kuwa wewe ndiwe Kristo, Mwana wake Mungu Mwenye uzima.*#Yoh. 1:49; 11:27; Mat. 16:16. 70Yesu akawajibu: Mimi sikuwachagua ninyi kumi na wawili? Tena mmoja wenu ni msengenyaji! 71Hapo alimsema Yuda wa Simoni, yule Iskariota; kwani huyo ndiye aliyemchongea halafu. Naye alikuwa miongoni mwao wale kumi na wawili.
Iliyochaguliwa sasa
Yohana 6: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.

: