Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka 13

13
Juteni!
1*Siku zilezile walikuwapo watu waliomsimulia ya Wagalilea, ambao Pilato alimwaga damu zao na kuzichanganya na damu za ng'ombe zao za tambiko. 2Akajibu akiwaambia: Mwadhani, Wagalilea hao walikuwa wakosaji kuwapita Wagalilea wote, maana wameteswa hivyo?#Yoh. 9:2. 3Nawaambiani: Sivyo, ila msipojuta nyote mtaangamia vivyo hivyo.#Sh. 7:13. 4Au wale kumi na wanane, uliowaangukia mnara kule Siloa na kuwaua, je? Mwadhani, wamekuwa wenye kulipizwa kuwapita wenyeji wote wa Yerusalemu? 5Nawaambiani: Sivyo, ila msipojuta nyote mtaangamia vivyo hivyo.
Mfano wa mkuyu.
6Akausema mfano huu: Mtu alikuwa na mkuyu uliopandwa mizabibuni kwake. Alipokuja kutafuta matunda yake hakuyaona.#Mat. 21:19. 7Kisha akamwambia mlimia mizabibu: Tazama, imepita miaka mitatu, tangu nilipoanza kuja kutafuta matunda ya mkuyu huu, lakini siyaoni. Basi, uukate! Hulizuiliani shamba? 8Lakini huyo akajibu akimwambia: Bwana, uuache mwaka huu tu, niuchimbie pembenipembeni, nikautilie mbolea!#2 Petr. 3:9,15. 9Labda utazaa matunda siku zitakazokuja. Lakini usipozaa, basi, utaukata.*
Kuponya siku ya mapumziko.
10Akawa akifundisha siku ya mapumziko katika nyumba moja ya kuombea.#Luk. 6:1-11. 11Mle nyumbani mkawa na mwanamke mwenye pepo aliyemwuguza miaka 18; kwa hiyo alikuwa amepindana, asiweze kunyoka kamwe. 12Yesu alipomwona akamwita, akamwambia: Mama, umefunguliwa huu unyonge wako; 13Kisha akambandikia mikono yake. Papo hapo akanyoka, akamtukuza Mungu.#Mar. 7:32. 14Lakini mkuu wa nyumba ya kuombea akamkasirikia Yesu, kwa sababu amemponya siku ya mapumziko, akawaambia watu waliokuwamo: Ziko siku sita za kufanya kazi; basi, mje siku hizo, mpate kuponywa, lakini msiponywe siku ya mapumziko!#2 Mose 20:9-10. 15Bwana akajibu akisema: Enyi wajanja, ninyi nyote hamwafungui ng'ombe au punda wenu zizini siku ya mapumziko na kuwapeleka, wanywe?#Luk. 14:5. 16Lakini huyu aliye mwana wa Aburahamu haikumpasa kufunguliwa siku ya mapumziko kifungo hiki, Satani alichomfunga miaka 18?#Luk. 19:9. 17Aliposema hayo, wabishi wake wakapatwa na soni wote, lakini wale watu wengi wote wakayafurahia mambo matukufu yote, aliyoyafanya.
Kipunje cha haradali.
(18-21: Mat. 13:31-33; Mar. 4:30-32.)
18Kisha akasema: Ufalme wa Mungu umefanana na nini? Niufananishe na nini? 19Umefanana na kipunje cha haradali, alichokitwaa mtu na kukitupia shambani kwake. Nacho hukua na kupata kuwa mti, hata ndege wa angani hutua katika matawi yake.
Chachu.
20Tena akasema: Ufalme wa Mungu niufananishe na nini? 21Umefanana na chachu, mwanamke akiitwaa, akaichanganya na pishi tatu za unga, mpaka ukachachwa wote.
Kuingia katika ufalme wa Mungu.
22Naye alipofanya mwendo wa kwenda Yerusalemu akapita mijini na vijijini akiwafundisha. 23Mtu alipomwuliza: Bwana, watu watakaookoka ni wachache tu? akamwambia: 24Gombeeni, mpate kuuingia mlango ulio mfinyu! Nawaambiani: Wengi watataka kuuingia, lakini hawataweza.#Mat. 7:13-14; Fil. 3:12. 25Tangu hapo, mwenye nyumba atakapoinuka na kuufunga mlango, ndipo, mtakapoanza kusimama nje na kuugonga mlango mkisema: Bwana, Bwana, tufungulie! Naye atajibu akiwaambia: Siwajui ninyi, mtokako.#Mat. 25:11-12. 26Ndipo, mtakapoanza kusema: Tumekula, tumekunywa machoni pako, nawe umetufundisha viwanjani petu.#Mat. 7:22-23. 27Ndipo, atakapowaambia ninyi: Siwajui, mtokako, ondokeni kwangu nyote mfanyao mapotovu!
(28-29: Mat. 8:11-12.)
28Ndiko, kitakakokuwa kilio na kukereza meno, mtakapowaona akina Aburahamu na Isaka na Yakobo na wafumbuaji wote, wamo katika ufalme wa Mungu, lakini ninyi wenyewe mtajiona, mmetupwa nje. 29Wako watakaotoka maawioni na machweoni kwa jua na upande wa kaskazini na wa kusini, nao watakaa chakulani katika ufalme wa Mungu.#Luk. 14:15. 30Tazameni, wako wa mwisho watakaokuwa wa kwanza, tena wako wa kwanza watakaokuwa wa mwisho.#Mat. 19:30.
Kuulilia mji wa Yerusalemu.
31Saa ileile wakawako Mafariseo waliomjia, wakamwambia: Toka hapa, ujiendee! kwani Herode anataka kukuua. 32Akawaambia: Nendeni, mkamwambie mbweha huyo: Tazama, leo na kesho nafukuza pepo na kuponya wagonjwa, nayo siku ya tatu mambo yangu yatamalizika. 33Lakini leo na kesho na kesho kutwa sharti niende, kwani haiwezekani, mfumbuaji auawe, isipokuwa Yerusalemu.
(34-35: Mat. 23:37-39.)
34Yerusalemu, Yerusalemu, unawaua wafumbuaji, ukawapiga mawe waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako, kama kuku anavyovikusanya vifaranga vyake mabawani! Lakini hamkutaka! 35Mtaona, Nyumba yenu ikiachwa, iwe peke yake! Nawaambiani: Hamtaniona tena mpaka siku ile, mtakaposema: Na atukuzwe ajaye kwa Jina la Bwana!#Sh. 118:26.

Iliyochaguliwa sasa

Luka 13: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia