Luka 20
20
Swali kuhusu mamlaka ya Isa
(Mathayo 21:23-27; Marko 11:27-33)
1Siku moja, Isa alipokuwa akifundisha watu Hekaluni na kuhubiri Habari Njema, viongozi wa makuhani, walimu wa Torati, pamoja na wazee wa watu wakamjia. 2Wakamuuliza, “Tuambie, unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Ni nani aliyekupa mamlaka haya?”
3Akawajibu, “Nami nitawauliza swali. Nijibuni: 4Je, ubatizo wa Yahya ulitoka mbinguni au kwa wanadamu?”
5Wakahojiana wao kwa wao na kusema, “Tukisema, ‘Ulitoka mbinguni,’ atatuuliza, ‘Mbona hamkumwamini?’ 6Lakini tukisema, ‘Ulitoka kwa wanadamu,’ watu wote watatupiga mawe, kwa sababu wanaamini kwamba Yahya alikuwa nabii.”
7Basi wakajibu, “Hatujui ulikotoka.”
8Isa akawaambia, “Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninatenda mambo haya.”
Mfano wa wapangaji waovu
(Mathayo 21:33-46; Marko 12:1-12)
9Akaendelea kuwaambia watu mfano huu: “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu, akalikodisha kwa wakulima fulani, kisha akasafiri kwa muda mrefu. 10Wakati wa mavuno ulipofika, akamtuma mtumishi wake kwa hao wapangaji ili wampe sehemu ya mavuno ya shamba la mizabibu. Lakini wale wakulima wakampiga, wakamfukuza mikono mitupu. 11Akamtuma mtumishi mwingine, huyo naye wakampiga, wakamfanyia mambo ya aibu na kumfukuza. 12Bado akamtuma na mwingine wa tatu, huyu pia wakamjeruhi na kumtupa nje ya shamba.
13“Basi yule mwenye shamba la mizabibu akasema, ‘Nifanye nini? Nitamtuma mwanangu mpendwa, huenda yeye watamheshimu.’
14“Lakini wale wapangaji walipomwona, wakasemezana wao kwa wao. Wakasema, ‘Huyu ndiye mrithi. Basi na tumuue ili urithi uwe wetu.’ 15Kwa hiyo wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamuua.
“Sasa basi yule mwenye shamba la mizabibu atawafanyia nini wapangaji hawa? 16Atakuja na kuwaua hao wapangaji, na kuwapa wapangaji wengine hilo shamba la mizabibu.”
Watu waliposikia hayo wakasema, “Mungu apishie mbali jambo hili lisitokee!”
17Lakini Isa akawakazia macho, akasema, “Basi ni nini maana ya yale yaliyoandikwa:
“ ‘Jiwe walilolikataa waashi,
limekuwa jiwe kuu la pembeni’?
18Kila mtu aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika vipande vipande, lakini yule litakayemwangukia atasagwa kabisa.”
19Walimu wa Torati na viongozi wa makuhani wakatafuta njia ya kumkamata mara moja, kwa sababu walifahamu kwamba amesema mfano huo kwa ajili yao. Lakini waliwaogopa watu.
Swali kuhusu kulipa kodi ya Kaisari
(Mathayo 22:15-22; Marko 12:13-17)
20Kwa hiyo wakawa wanamchunguza na kutuma wapelelezi waliojifanya kuwa wenye haki. Walitaka kumtega kwa maneno yake, ili wampeane katika uwezo na mamlaka ya mtawala. 21Hivyo wale wapelelezi wakamuuliza, “Mwalimu, tunajua unasema na kufundisha yaliyo kweli wala humpendelei mtu, bali wafundisha njia ya Mungu katika kweli. 22Je, ni halali sisi kulipa kodi kwa Kaisari, au la?”
23Lakini Isa akatambua hila yao, akawaambia, 24“Nionesheni dinari. Je, sura hii na maandishi haya yaliyo juu yake ni vya nani?”
Wakamjibu, “Ni vya Kaisari.”
25Akawaambia, “Basi mpeni Kaisari kilicho cha Kaisari, naye Mungu mpeni kilicho cha Mungu.”
26Wakashindwa kumkamata kwa yale aliyokuwa amesema hadharani. Nao wakashangazwa mno na majibu yake, wakanyamaza.
Ndoa wakati wa ufufuo
(Mathayo 22:23-33; Marko 12:18-27)
27Baadhi ya Masadukayo, wale wasemao kuwa hakuna ufufuo wa wafu, wakamjia Isa na kumuuliza, 28“Mwalimu, Musa alituandikia kwamba kama ndugu wa mtu akifa na kumwacha mkewe bila mtoto, basi huyo mtu inampasa amwoe huyo mjane ili amzalie ndugu yake watoto. 29Basi kulikuwa na ndugu saba. Yule wa kwanza akaoa, akafa bila kuzaa mtoto. 30Kisha yule wa pili akamwoa huyo mjane, naye akafa bila mtoto, 31naye wa tatu pia akamwoa. Vivyo hivyo ndugu wote saba wakawa wamemwoa huyo mwanamke, na wote wakafa pasipo yeyote kupata mtoto. 32Mwishowe, yule mwanamke naye akafa. 33Sasa basi, siku ya ufufuo huyo mwanamke atakuwa mke wa nani, maana aliolewa na ndugu wote saba?”
34Isa akawajibu, “Katika maisha haya watu huoa na kuolewa. 35Lakini wale ambao wamehesabiwa kwamba wanastahili kupata nafasi katika ulimwengu ule na katika ufufuo wa wafu, hawaoi wala hawaolewi. 36Hawa hawawezi kufa tena, kwa maana wao ni kama malaika. Wao ni watoto wa Mungu, kwa sababu ni watoto wa ufufuo. 37Hata Musa alidhihirisha kuwa wafu wanafufuka, kwa habari ya kile kichaka kilichokuwa kikiwaka moto bila kuteketea, alipomwita Mwenyezi Mungu, ‘Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo.’ 38Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai, kwa kuwa kwake wote ni hai.”
39Baadhi ya walimu wa Torati wakasema, “Mwalimu, umesema sawasawa kabisa!”
40Baada ya hayo hakuna mtu aliyethubutu kumuuliza maswali tena.
Al-Masihi ni Mwana wa nani?
(Mathayo 22:41-46; Marko 12:35-37)
41Kisha Isa akawaambia, “Imekuwaje basi wao husema Al-Masihi#20:41 Al-Masihi maana yake Aliyetiwa mafuta. ni Mwana wa Daudi? 42Daudi mwenyewe anasema katika Kitabu cha Zaburi:
“ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu:
“Keti mkono wangu wa kuume,
43hadi nitakapowaweka adui zako
chini ya miguu yako.” ’
44Ikiwa Daudi anamwita yeye ‘Bwana,’ basi atakuwaje mwanawe?”
Isa atahadharisha kuhusu walimu wa Torati
(Mathayo 23:1-36; Marko 12:38-40)
45Wakati watu wote walikuwa wanamsikiliza, Isa akawaambia wanafunzi wake, 46“Jihadharini na walimu wa Torati. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa kwa heshima masokoni. Hupenda kukaa kwenye viti vya mbele katika masinagogi#20:46 Nyumba za ibada na mafunzo., na kukaa kwenye nafasi za heshima katika karamu. 47Wao hula nyumba za wajane, na ili waonekane kuwa wema, wanasali sala ndefu. Watu kama hawa watapata hukumu iliyo kuu sana.”
Iliyochaguliwa sasa
Luka 20: ONMM
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.

: