Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Amosi UTANGULIZI

UTANGULIZI
Amosi aliishi kabla ya manabii wengine wote ambao tumeachiwa vitabu vyao. Yeye alizaliwa katika utawala wa kusini wa Yuda lakini akaitwa kuhudumu katika utawala wa kaskazini mnamo mwaka 750 K.K.
Wakati huu ulikuwa wa fanaka na maendeleo ya uchumi na usalama. Lakini Amosi aliona dhahiri kwamba hali hiyo iliwafaa matajiri na uchumi huo ulipatikana kwa dhuluma na ukandamizaji wa maskini. Utekelezaji wa mambo ya kidini ulikuwa wa unafiki, na usalama wa kisiasa haukuwa thabiti. Ulichanganyika na kila namna ya ukosefu katika jamii.
Amosi aliikabili hali hiyo, akashutumu ukosefu wa haki katika jamii kwa uhodari wa pekee. Amosi aliwaambia watu kwamba Mungu atawaadhibu. Mwito wake kwa viongozi wazingatie haki haukupokelewa vizuri. Alikatazwa kufanya huduma yake ya kinabii huko Betheli.

Iliyochaguliwa sasa

Amosi UTANGULIZI: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia