Mwanzo 13:14-18
Mwanzo 13:14-18 BHN
Baada ya Loti kujitenga na Abramu, Mwenyezi-Mungu akamwambia Abramu, “Angalia toka hapo ulipo utazame pande zote: Kaskazini, Kusini, Mashariki na Magharibi. Nchi hii yote unayoiona nitakupa wewe na wazawa wako iwe yenu milele. Wazawa wako nitawafanya wawe wengi wasiohesabika, kama vile mavumbi ya nchi yasivyoweza kuhesabika! Basi, inuka uitembelee nchi hii katika mapana na marefu, kwani nitakupa wewe.” Kwa hiyo, Abramu akangoa hema, akaenda kukaa karibu na mialoni ya Mamre kule Hebroni; huko akamjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu.