Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waebrania 7:18-25

Waebrania 7:18-25 BHN

Basi, ile amri ya zamani ilifutwa kwa sababu ilikuwa hafifu na isiyofaa kitu. Maana sheria ya Mose haikuweza kukamilisha jambo lolote. Lakini sasa, mahali pake pamewekwa tumaini lililo bora zaidi ambalo kwalo tunaweza kumkaribia Mungu. Zaidi ya hayo, hapa pana kiapo cha Mungu. Wakati wale wengine walipofanywa makuhani hapakuwako kiapo. Lakini Yesu alifanywa kuhani kwa kiapo wakati Mungu alipomwambia: “Bwana ameapa, wala hatabadili nia yake: ‘Wewe ni kuhani milele.’” Basi, kutokana na tofauti hii, Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi. Tena: Hao makuhani wengine walikuwa wengi kwa sababu walikufa na hawakuweza kuendelea na kazi yao. Lakini Yesu si kama wao, yeye anaishi milele; ukuhani wake hauondoki kwake. Hivyo, yeye anaweza daima kuwaokoa kabisa wote wanaomwendea Mungu kwa njia yake, maana yeye anaishi milele kuwaombea kwa Mungu.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Waebrania 7:18-25