Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hosea 13:1-11

Hosea 13:1-11 BHN

Waefraimu waliponena, watu walitetemeka; Waefraimu walikuwa na uwezo mkubwa huko Israeli, lakini walianza kumwabudu Baali, wakajiletea kifo. Waefraimu wameendelea kutenda dhambi, wakajitengenezea sanamu za kusubu, sanamu zilizotengenezwa kwa ustadi wao, zote zikiwa kazi ya mafundi. Wanasema, “Haya zitambikieni!” Wanaume wanabusu ndama! Basi, watatoweka kama ukungu wa asubuhi, kama umande utowekao upesi; kama makapi yanayopeperushwa mahali pa kupuria, kama moshi unaotoka katika bomba. Mwenyezi-Mungu asema: “Lakini mimi, Mwenyezi-Mungu, ni Mungu wenu, ambaye niliwatoa nchini Misri; hamna mungu mwingine ila mimi, wala hakuna awezaye kuwaokoeni. Ni mimi niliyewatunza mlipokuwa jangwani, katika nchi iliyokuwa ya ukame. Lakini mlipokwisha kula na kushiba, mlianza kuwa na kiburi, mpaka mkanisahau. Basi, nitakuwa kama simba kwenu nyote; nitawavizieni kama chui njiani. Nitawarukieni kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake. Nitawararua vifua vyenu na kuwala papo hapo kama simba; nitawararua vipandevipande kama mnyama wa porini. “Nitawaangamiza, enyi Waisraeli. Nani ataweza kuwasaidia? Yuko wapi sasa mfalme wenu awaokoe? Wako wapi wale wakuu wenu wawalinde? Nyinyi ndio mlioomba: ‘Tupatie mfalme na wakuu watutawale.’ Kwa hasira yangu mimi nikawapa mfalme, kisha nikamwondoa kwa ghadhabu yangu.

Soma Hosea 13