Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yobu 23

23
Jibu la Yobu
1Kisha Yobu akajibu:
2“Leo pia lalamiko langu ni chungu.
Napata maumivu na kusononeka.
3Laiti ningejua mahali nitakapompata Mungu!
Ningeweza kwenda hata karibu naye.
4Ningeleta kesi yangu mbele yake,
na kumtolea hoja yangu.
5Ningeweza kujua atakachonijibu,
na kuelewa atakachoniambia.
6Je, angeshindana nami kwa nguvu zake zote?
La! Bila shaka angenisikiliza.
7Yeye aweza kuzungumza na mtu mnyofu,
Mungu, hakimu wangu angeamua kuwa sina hatia milele.
8“Tazama, nakwenda mbele, lakini simpati,
narudi nyuma, lakini siwezi kumwona.
9Namtafuta upande wa kushoto lakini simwoni;
nageukia kulia, lakini siwezi kumwona.
10Lakini yeye anajua njia ninayofuata;
atakapomaliza kunijaribu
nitatoka humo safi kama dhahabu.
11Nafuata nyayo zake kwa uaminifu
njia yake nimeishikilia wala sikupinda.
12Kamwe sijaacha kushika amri yake,
maneno yake nimeyatunza moyoni mwangu.
13Lakini yeye habadiliki, nani awezaye kumgeuza?
Analotaka, ndilo analofanya!
14Atanijulisha yote aliyonipangia;
na mengi kama hayo yamo akilini mwake.
15Hivyo, natetemeka kwa hofu mbele yake;
hata nikifikiria tu napatwa na woga.
16Mungu ameufanya moyo wangu ufifie,
Mungu Mwenye Nguvu amenitia hofu.
17Maana nimekumbwa na giza,
na giza nene limetanda usoni mwangu.#23:17 maana katika makala ya Kiebrania si dhahiri. Wengine wanaelewa: Sikuangamizwa kabla usiku haujaingia, lakini yeye (Mungu) hakuniondolea giza.

Iliyochaguliwa sasa

Yobu 23: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia