Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 6:20-24

Methali 6:20-24 BHN

Mwanangu, shika maagizo ya baba yako, wala usisahau mafundisho ya mama yako; yaweke daima moyoni mwako, yafunge shingoni mwako. Yatakuongoza njiani mwako, yatakulinda wakati ulalapo, yatakushauri uwapo macho mchana. Maana amri hiyo ni taa, na sheria hiyo ni mwanga. Maonyo hayo na nidhamu yatuweka njiani mwa uhai. Yatakulinda mbali na mwanamke mbaya, yatakuepusha na maneno matamu ya mwanamke mgeni.

Soma Methali 6