Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 132

132
Sifa ya nyumba ya Mungu
(Wimbo wa Kwenda Juu)
1Ee Mwenyezi-Mungu, mkumbuke Daudi,
kumbuka taabu zote alizopata.
2Ukumbuke ahadi aliyokupa, ee Mwenyezi-Mungu,
kiapo alichokuapia, ewe Mwenye Nguvu wa Yakobo:
3“Sitaingia ndani ya nyumba yangu,
wala kulala kitandani mwangu;
4sitakubali kulala usingizi,
wala kusinzia;
5mpaka nikupatie wewe Mwenyezi-Mungu mahali pa kukaa,
makao yako, ewe Mwenye Nguvu wa Yakobo!”
6Huko Efratha tulisikia habari za sanduku la agano,
tukalikuta katika mashamba ya Yearimu.
7“Haya! Twende nyumbani kwa Mungu,
tuabudu mbele ya kiti chake cha enzi!”
8Inuka ee Mwenyezi-Mungu, nenda kwenye maskani yako;
inuka pamoja na sanduku la agano la uwezo wako!
9Makuhani wako wawe waadilifu daima;
na waaminifu wako wapige vigelegele vya furaha!
10Kwa ajili ya Daudi, mtumishi wako,
usimkatae huyo mfalme uliyemweka wakfu.
11 # Taz Zab 89:3-4; Mate 2:30 Mwenyezi-Mungu alimwapia Daudi kiapo thabiti,
kiapo ambacho hatakibatilisha:
“Nitamtawaza mmoja wa wazawa wako mwenyewe,
kuwa mfalme baada yako.
12Watoto wako wakishika agano langu,
na kuzingatia mafundisho nitakayowapa,
watoto wao pia watakuwa wafalme kama wewe.”
13Mwenyezi-Mungu ameuchagua mji wa Siyoni,
ametaka uwe makao yake:
14“Hapa ndipo nitakapokaa milele,
ndipo maskani yangu maana nimepachagua.
15Nitaubariki sana mji wa Siyoni kwa mahitaji yake;
nitawashibisha chakula maskini wake.
16Nitawafanikisha makuhani wake kwa wokovu;#132:16 … kwa wokovu: Mstari huu wa kwanza wa aya hii haueleweki; wengine wana ushindi badala ya wokovu.
waaminifu wake watapiga vigelegele vya furaha.
17Humo nitamchipusha mfalme shujaa wa ukoo wa Daudi:
Kama taa iwakayo nitamtegemeza mfalme niliyemteua.
18Maadui zake nitawavika aibu;
lakini yeye nitamvika fahari ya kifalme.”

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 132: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia