Zaburi 24:7-10
Zaburi 24:7-10 BHN
Fungukeni enyi milango; fungukeni enyi milango ya kale, ili Mfalme mtukufu aingie. Ni nani huyo Mfalme mtukufu? Ni Mwenyezi-Mungu, mwenye nguvu na uwezo; Mwenyezi-Mungu, mwenye uwezo vitani. Fungukeni enyi malango, fungukeni enyi milango ya kale, ili Mfalme mtukufu aingie. Ni nani huyo Mfalme mtukufu? Ni Mwenyezi-Mungu, wa majeshi, yeye ndiye Mfalme mtukufu.