Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zekaria 10:4-12

Zekaria 10:4-12 BHN

Kwa ukoo wa Yuda kutatokea: Watawala wa kila namna, viongozi imara kama jiwe kuu la msingi, walio thabiti kama kigingi cha hema, wenye nguvu kama upinde wa vita. Watu wa Yuda watakuwa kama mashujaa vitani watawakanyaga maadui zao katika tope njiani. Watapigana kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nipo pamoja nao; nao watawaaibisha hata wapandafarasi. “Watu wa Yuda nitawaimarisha; nitawaokoa wazawa wa Yosefu. Nitawarejesha makwao kwa maana nawaonea huruma, nao watakuwa kana kwamba sikuwa nimewakataa. Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, nami nitayasikiliza maombi yao. Watu wa Efraimu watakuwa kama mashujaa vitani; watajaa furaha kama waliokunywa divai. Watoto wao wataona hayo na kufurahi, watajaa furaha mioyoni kwa sababu yangu Mwenyezi-Mungu. “Nitawaita watu wangu na kuwakusanya pamoja; nimekusudia kuwakomboa, nao watakuwa wengi kama hapo awali. Japo niliwatawanya kati ya mataifa, hata hivyo, watanikumbuka wakiwa humo. Nao pamoja na watoto wao wataishi na kurudi majumbani mwao. Nitawarudisha kutoka nchini Misri, nitawakusanya kutoka Ashuru; nitawaleta nchini Gileadi na Lebanoni, nao watajaa kila mahali nchini. Watapitia katika bahari ya mateso, nami nitayapiga mawimbi yake, na vilindi vya maji ya mto Nili vitakauka. Kiburi cha Ashuru kitavunjwa na nguvu za Misri zitatoweka. Mimi nitawaimarisha watu wangu, nao watanitii na kuishi kwa kunipendeza. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Soma Zekaria 10

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zekaria 10:4-12