1 Yohane 1:8-10
1 Yohane 1:8-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Tukisema kwamba hatuna dhambi, tunajidanganya wenyewe, na ukweli haumo ndani yetu. Lakini tukiziungama dhambi zetu, basi, Mungu ni mwaminifu na mwadilifu, naye atatusamehe dhambi zetu na kututakasa uovu wote. Tukisema kwamba hatujatenda dhambi, tutakuwa tumemfanya Mungu mwongo, na neno lake halimo ndani yetu.
1 Yohane 1:8-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tukisema kwamba hatuna dhambi, tunajidanganya wenyewe, wala kweli haimo ndani yetu. Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kututakasa na udhalimu wote. Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, tunamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo ndani yetu.
1 Yohane 1:8-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu.
1 Yohane 1:8-10 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe wala kweli haimo ndani yetu. Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha kutokana na udhalimu wote. Tukisema hatujatenda dhambi, twamfanya yeye kuwa mwongo na neno lake halimo ndani yetu.