1 Yohane 5:13-15
1 Yohane 5:13-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Nawaandikieni mpate kujua kwamba mnao uhai wa milele nyinyi mnaoamini kwa jina la Mwana wa Mungu. Na sisi tuko thabiti mbele ya Mungu kwani tuna hakika kwamba tukimwomba chochote kadiri ya matakwa yake, yeye hutusikiliza. Yeye hutusikiliza kila tunapomwomba; na kwa vile tunajua kwamba yeye hutusikiliza kila tunapomwomba, twajua pia kwamba hutupatia yote tunayomwomba.
1 Yohane 5:13-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu. Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tunapoomba chochote, tunajua kwamba tumetimiziwa zile haja tulizomwomba.
1 Yohane 5:13-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu. Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.
1 Yohane 5:13-15 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Nawaandikia mambo haya ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu ili mpate kujua ya kuwa mnao uzima wa milele. Huu ndio ujasiri tulio nao tunapomkaribia Mungu, kwamba tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Nasi kama tunajua atusikia, lolote tuombalo, tunajua kwamba tumekwisha kupata zile haja tulizomwomba.