1 Timotheo 5:17-20
1 Timotheo 5:17-20 Biblia Habari Njema (BHN)
Viongozi wa kanisa wanaowaongoza watu vizuri wanastahili kupata riziki maradufu, hasa wale wanaofanya bidii katika kuhubiri na kufundisha. Maana Maandiko Matakatifu yasema: “Usimfunge ng'ombe kinywa anapopura nafaka,” na tena “Mfanyakazi astahili malipo yake.” Usikubali kupokea mashtaka dhidi ya mzee yasipowakilishwa na mashahidi wawili au watatu. Wale wanaotenda dhambi waonye hadharani, ili wengine wapate kuogopa.
1 Timotheo 5:17-20 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kutoa unabii na kufundisha. Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ng'ombe apurapo nafaka. Na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake. Usikubali mashitaka juu ya mzee, ila kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu. Wale wadumuo kutenda dhambi uwakemee mbele ya wote, ili na wengine waogope.
1 Timotheo 5:17-20 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha. Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ng’ombe apurapo nafaka. Na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake. Usikubali mashitaka juu ya mzee, ila kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu. Wale wadumuo kutenda dhambi uwakemee mbele ya wote, ili na wengine waogope.
1 Timotheo 5:17-20 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Wazee wa kundi la waumini wanaoongoza shughuli za kundi hilo vizuri wanastahili heshima mara mbili, hasa wale ambao kazi yao ni kuhubiri na kufundisha. Kwa maana Maandiko husema, “Usimfunge maksai kinywa apurapo nafaka,” tena, “Mfanyakazi anastahili mshahara wake.” Usiendekeze mashtaka dhidi ya mzee isipokuwa yawe yameletwa na mashahidi wawili au watatu. Wale wanaodumu katika dhambi uwakemee hadharani, ili wengine wapate kuogopa.