2 Mambo ya Nyakati 5:13-14
2 Mambo ya Nyakati 5:13-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
hata ikawa, wenye panda na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakisikizisha sauti moja ya kumsifu na kumshukuru BWANA nao wakipaza sauti pamoja na panda na matoazi na vinanda, wakimsifu BWANA, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele; ndipo nyumba ikajawa na wingu, naam, nyumba ya BWANA, hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya lile wingu; kwa kuwa nyumba ya Mungu imejaa utukufu wa BWANA.
2 Mambo ya Nyakati 5:13-14 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wapiga tarumbeta na waimbaji wakaungana katika sauti linganifu, ikawa kama vile ni sauti moja, wakimsifu na kumshukuru BWANA, nao alipoinua sauti zao pamoja na tarumbeta na matoazi na vyombo vingine vya uimbaji, wakamsifu BWANA wakisema: “Yeye ni mwema; upendo wake unadumu milele.” Ndipo Hekalu la BWANA likajazwa na wingu, nao makuhani hawakuweza kufanya huduma yao kwa sababu ya lile wingu, kwa kuwa utukufu wa BWANA ulijaza Hekalu la Mungu.
2 Mambo ya Nyakati 5:13-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Waimbaji, huku wakifuatiwa na sauti linganifu za tarumbeta, matoazi na vyombo vingine vya muziki, walimsifu Mwenyezi-Mungu wakiimba: “Maana yeye ni mwema, na fadhili zake zadumu milele.” Wakati huo nyumba ya Mwenyezi-Mungu ilijazwa wingu. Nao makuhani walishindwa kuhudumu humo kwa sababu ya wingu hilo, maana utukufu wa Mwenyezi-Mungu uliijaza nyumba ya Mungu.
2 Mambo ya Nyakati 5:13-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)