2 Wakorintho 11:14-15
2 Wakorintho 11:14-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.
2 Wakorintho 11:14-15 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wala hii si ajabu, kwa kuwa hata Shetani mwenyewe hujigeuza aonekane kama malaika wa nuru. Kwa hiyo basi si ajabu, kama watumishi wa Shetani nao hujigeuza ili waonekane kama watumishi wa haki. Mwisho wao utakuwa sawa na matendo yao yanavyostahili.
2 Wakorintho 11:14-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Wala si ajabu, maana hata Shetani mwenyewe hujisingizia kuwa malaika wa mwanga! Kwa hiyo si jambo la kushangaza ikiwa na hao watumishi wake wanajisingizia kuwa watumishi wa haki. Mwisho wao watapata kile wanachostahili kufuatana na matendo yao.
2 Wakorintho 11:14-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)