2 Wakorintho 3:18
2 Wakorintho 3:18 Biblia Habari Njema (BHN)
Basi, sisi sote ambao nyuso zetu hazikufunikwa, tunaona kama katika kioo, utukufu wa Bwana; tunabadilishwa tufanane zaidi na huo mfano wake kwa utukufu mwingi zaidi. Hiyo ni kazi yake Roho wa Bwana.
2 Wakorintho 3:18 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nasi sote, tukiwa na nyuso zisizotiwa utaji tunadhihirisha utukufu wa Bwana, kama kwenye kioo. Nasi tunabadilishwa ili tufanane naye, toka utukufu hadi utukufu mkuu zaidi, utokao kwa Bwana, ambaye ndiye Roho.
2 Wakorintho 3:18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.
2 Wakorintho 3:18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)