2 Wafalme 7:1
2 Wafalme 7:1 Biblia Habari Njema (BHN)
Elisha akamjibu, “Sikiliza neno la Mwenyezi-Mungu: Kesho wakati kama huu, humu Samaria kilo tatu za unga bora wa ngano zitagharimu fedha shekeli moja ya fedha, na kilo sita za shayiri kadhalika zitagharimu fedha shekeli moja.”
2 Wafalme 7:1 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Elisha akasema, Lisikieni neno la BWANA; BWANA asema hivi, Kesho panapo saa hii, kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, langoni pa Samaria.
2 Wafalme 7:1 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Elisha akasema, Lisikieni neno la BWANA; BWANA asema hivi, Kesho panapo saa hii, kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, langoni pa Samaria.
2 Wafalme 7:1 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Elisha akasema, “Sikiliza neno la BWANA. Hivi ndivyo asemavyo BWANA: Wakati kama huu kesho, kipimo kimoja cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli moja ya fedha, na vibaba viwili vya shayiri kwa shekeli moja ya fedha katika lango la Samaria.”