2 Timotheo 4:3-4
2 Timotheo 4:3-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajikusanyia waalimu wengi, watakaowaambia yale tu masikio yao yanataka kusikia; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.
2 Timotheo 4:3-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Utakuja wakati ambapo watu hawatasikiliza mafundisho ya kweli, ila watafuata tamaa zao wenyewe na kujikusanyia waalimu tele watakaowaambia mambo yale tu ambayo masikio yao yako tayari kusikia. Watakataa kuusikia ukweli, watageukia hadithi za uongo.
2 Timotheo 4:3-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.
2 Timotheo 4:3-4 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Maana wakati utakuja watu watakapokataa kuyakubali mafundisho yenye uzima. Badala yake, ili kutimiza tamaa zao wenyewe, watajikusanyia idadi kubwa ya walimu wapate kuwaambia yale ambayo masikio yao yanayowasha yanatamani kuyasikia. Watakataa kusikiliza kweli na kuzigeukia hadithi za uongo.