Danieli 5:25-28
Danieli 5:25-28 Biblia Habari Njema (BHN)
“Maandishi yenyewe ni: ‘MENE, MENE, TEKELI, PARSINI.’ Na hii ndiyo maana yake: MENE maana yake, Mungu amehesabu siku za ufalme wako na kuukomesha. TEKELI maana yake, wewe umepimwa katika mizani, nawe ukaonekana huna uzito wowote. PERESI maana yake, ufalme wako umegawanywa kati ya Wamedi na Wapersi.”
Danieli 5:25-28 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE, MENE, TEKELI, NA PERESI. Na tafsiri ya maneno haya ni hii; MENE, Mungu ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha. TEKELI, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka. PERESI, ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na Waajemi.
Danieli 5:25-28 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE, MENE, TEKELI, NA PERESI. Na tafsiri ya maneno haya ni hii; MENE, Mungu ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha. TEKELI, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka. PERESI, ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na Waajemi.
Danieli 5:25-28 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Haya ndiyo maneno yaliyoandikwa: mene, mene, tekeli na peresi “Hii ndiyo maana ya maneno haya: “ Mene : Mungu amezihesabu siku za utawala wako na kuukomesha. Tekeli : Wewe umepimwa katika mizani na umeonekana umepungua. Peresi : Ufalme wako umegawanywa na kupewa Wamedi na Waajemi.”