Kumbukumbu la Sheria 18:10-11
Kumbukumbu la Sheria 18:10-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.
Kumbukumbu la Sheria 18:10-11 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Asionekane mtu yeyote miongoni mwenu ampitishaye mwanawe au binti yake katika moto, atakayefanya uaguzi, ulozi, anayetabiri nyakati, anayejishughulisha na uchawi, wala arogaye kwa kupiga mafundo, wala mwaguzi au anayeabudu mizimu, wala awaombaye wafu.
Kumbukumbu la Sheria 18:10-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Pasiwe mtu yeyote miongoni mwenu atakayemtambika mtoto wake wa kiume au wa kike kwa moto, wala mtu apigaye ramli, wala mwaguzi, wala mpiga bao, wala mchawi, wala mlozi, wala mwenye kutaka kauli kwa mizimu na pepo au kutoka kwa wafu.
Kumbukumbu la Sheria 18:10-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)