Kumbukumbu la Sheria 30:9
Kumbukumbu la Sheria 30:9 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ndipo BWANA Mungu wako atakapokufanikisha sana katika kazi zote za mikono yako na katika uzao wa tumbo lako, wadogo wa mifugo yako na mazao ya nchi yako. BWANA atakufurahia tena na kukufanikisha, kama alivyowafurahia baba zako
Kumbukumbu la Sheria 30:9 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu atawafanya mfanikiwe katika kila mtakalofanya; mtakuwa na watoto wengi na ng'ombe wengi na mashamba yenu yatatoa mazao. Maana atapenda tena kuwafanya mfanikiwe kama vile alivyopenda kuwafanikisha wazee wenu
Kumbukumbu la Sheria 30:9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na BWANA, Mungu wako, atakufanya uwe na wingi wa uheri katika kazi yote ya mkono wako, katika uzao wa tumbo lako, na katika uzao wa ng'ombe wako, na katika uzao wa nchi yako; kwa kuwa BWANA atafurahi tena juu yako kwa wema, kama alivyofurahi juu ya baba zako
Kumbukumbu la Sheria 30:9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na BWANA, Mungu wako, atakufanya uwe na wingi wa uheri katika kazi yote ya mkono wako, katika uzao wa tumbo lako, na katika uzao wa ng’ombe wako, na katika uzao wa nchi yako; kwa kuwa BWANA atafurahi tena juu yako kwa wema, kama alivyofurahi juu ya baba zako