Kumbukumbu la Sheria 31:7
Kumbukumbu la Sheria 31:7 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha Mose akamwita Yoshua, akamwambia mbele ya watu wote wa Israeli, “Uwe Imara na hodari, maana wewe utawaongoza watu hawa kwenda kuimiliki nchi ambayo Mwenyezi-Mungu aliwaahidi babu zao; nawe utawakabidhi waimiliki.
Kumbukumbu la Sheria 31:7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kisha Mose akamwita Yoshua na akamwambia mbele ya Israeli wote, “Uwe imara na moyo wa ushujaa, kwa kuwa ni lazima uende na watu hawa katika nchi ile BWANA aliyowaapia baba zao kuwapa, nawe ni lazima uwagawie kama urithi wao.
Kumbukumbu la Sheria 31:7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Musa akamwita Yoshua, akamwambia machoni pa Israeli wote, Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana utakwenda pamoja na watu hawa hata nchi BWANA aliyowaapia baba zao, ya kwamba atawapa; nawe utawarithisha.
Kumbukumbu la Sheria 31:7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)