Mhubiri 12:6-7
Mhubiri 12:6-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kabla haijakatika kamba ya fedha; Au kuvunjwa bakuli la dhahabu; Au mtungi kuvunjika kisimani; Au gurudumu kuvunjika birikani; Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.
Mhubiri 12:6-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Wakati huo uzi wa dhahabu utakatika, bakuli la dhahabu litapasuka, mtungi wa maji utavunjikia kisimani, kadhalika na gurudumu la kuvutia maji. Nawe vumbi utarudia udongoni ulimotolewa na roho yako itamrudia Mungu aliyeiumba.
Mhubiri 12:6-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kabla haijakatika kamba ya fedha; Au kuvunjwa bakuli la dhahabu; Au mtungi kuvunjika kisimani; Au gurudumu kuvunjika birikani; Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.
Mhubiri 12:6-7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mkumbuke Muumba wako: kabla haijakatika kamba ya fedha, au bakuli la dhahabu halijavunjika; kabla mtungi kuvunjika kwenye chemchemi, au gurudumu kuvunjika kisimani, nayo mavumbi kurudi ardhini yalikotoka, na roho kurudi kwa Mungu aliyeitoa.