Kutoka 29:45-46
Kutoka 29:45-46 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na mimi nitakaa kati ya wana wa Israeli, nami nitakuwa Mungu wao. Nao watanijua kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wao, niliyewatoa katika nchi ya Misri, nipate kukaa kati yao; ni mimi BWANA Mungu wao.
Shirikisha
Soma Kutoka 29Kutoka 29:45-46 Biblia Habari Njema (BHN)
Nitaishi kati ya Waisraeli, nami nitakuwa Mungu wao. Hapo ndipo watakapotambua kuwa mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili niishi kati yao. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wao.
Shirikisha
Soma Kutoka 29