Kutoka 37:1-2
Kutoka 37:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Bezaleli alitengeneza sanduku kwa mbao za mjohoro; urefu wake ulikuwa sentimita 110, upana sentimita 66, na kimo chake sentimita 66. Alilipaka dhahabu safi ndani na nje, na kulifanyia ukingo wa dhahabu pande zote.
Kutoka 37:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kisha Bezaleli akalifanya lile sanduku la mti wa mshita, urefu wake ulikuwa dhiraa mbili na nusu, na upana wake ulikuwa dhiraa moja na nusu, na kwenda juu kwake kulikuwa ni dhiraa moja na nusu; akalifunika dhahabu safi, ndani na nje, akafanya na ukingo wa dhahabu kulizunguka pande zote.
Kutoka 37:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kisha Bezaleli akalifanya lile sanduku la mti wa mshita, urefu wake ulikuwa dhiraa mbili na nusu, na upana wake ulikuwa dhiraa moja na nusu, na kwenda juu kwake kulikuwa ni dhiraa moja na nusu; akalifunika dhahabu safi, ndani na nje, akafanya na ukingo wa dhahabu kulizunguka pande zote.
Kutoka 37:1-2 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Bezaleli akatengeneza Sanduku la mbao za mshita: urefu wake ulikuwa dhiraa mbili na nusu, upana wake dhiraa moja na nusu, na kimo chake dhiraa moja na nusu. Akalifunika kwa dhahabu safi ndani na nje, na kulizungushia ukingo wa dhahabu.