Ezekieli 17:22-24
Ezekieli 17:22-24 Biblia Habari Njema (BHN)
Bwana Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Mimi mwenyewe nitachukua kisehemu cha ncha ya juu ya mwerezi, naam, nitavunja tawi changa kutoka matawi yake ya juu na kulipanda juu ya mlima mrefu sana. Naam, nitalipanda juu ya mlima mrefu wa Israeli ili lichanue na kuzaa matunda. Litakuwa mwerezi mzuri, na ndege wa aina zote watakaa chini yake pia watajenga viota vyao katika matawi yake. Ndipo miti yote nchini itajua kuwa mimi Mwenyezi-Mungu huiporomosha miti mirefu na kuikuza miti mifupi. Mimi hukausha miti mibichi na kustawisha miti mikavu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema hayo na nitayafanya.”
Ezekieli 17:22-24 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Bwana MUNGU asema hivi; Mimi nami nitakitwaa kilele kirefu cha mwerezi, na kukipandikiza mahali; na katika vitawi vyake vilivyo juu nitatwaa kitawi kimoja kilicho chororo, nami nitakipanda juu ya mlima mrefu ulioinuka sana; juu ya mlima wa mahali palipoinuka pa Israeli nitakipanda; nacho kitatoa matawi, na kuzaa matunda, nao utakuwa mwerezi mzuri; na chini yake watakaa ndege wa kila namna ya mbawa; katika uvuli wa matawi yake watakaa. Na miti yote ya mashamba itajua ya kuwa mimi, BWANA, nimeushusha chini mti mrefu, na kuuinua mti mfupi, na kuukausha mti mbichi, na kuusitawisha mti mkavu; mimi, BWANA, nimenena, nami nimelitenda jambo hili.
Ezekieli 17:22-24 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Ezekieli 17:22-24 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“ ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Mimi mwenyewe nitachukua chipukizi kutoka kwenye kilele cha juu sana cha mwerezi na kukipanda, nitavunja kitawi kichanga kutoka matawi yake ya juu kabisa na kukipanda juu ya mlima mrefu ulioinuka sana. Katika vilele vya mlima mrefu wa Israeli nitakipanda, kitatoa matawi na kuzaa matunda na kuwa mwerezi mzuri sana. Ndege wa kila aina wataweka viota vyao ndani yake, nao watapata makazi katika kivuli cha matawi yake. Miti yote ya kondeni itajua kuwa Mimi BWANA ninaishusha miti mirefu na kuikuza miti mifupi kuwa miti mirefu. Mimi naikausha miti mibichi na kuifanya miti mikavu istawi. “ ‘Mimi BWANA nimesema, nami nitatenda.’ ”