Ezekieli 19:1-14
Ezekieli 19:1-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tena uwaombolezee wakuu wa Israeli, useme, Mama yako alikuwa nini? Simba mke; alijilaza kati ya simba, kati ya wanasimba aliwalisha watoto wake. Akamlea mtoto mmoja katika watoto wake, akawa mwanasimba, akajifunza kuwinda mawindo, akala watu. Mataifa nao wakapata habari zake, akanaswa katika rima lao, wakamchukua kwa kulabu mpaka nchi ya Misri. Basi mamaye alipoona kwamba amemngoja, na tumaini lake limepotea, akatwaa mtoto mwingine katika watoto wake, akamfanya mwanasimba. Naye akaenda huku na huko kati ya simba, akawa mwanasimba, akajifunza kuwinda mawindo, akala watu. Akayajua majumba yao, akaiharibu miji yao; nchi ikawa ukiwa, na vyote vilivyomo, kwa sababu ya mshindo wa kunguruma kwake. Ndipo mataifa wakajipanga juu yake pande zote toka nchi zote; wakaunda wavu wao juu yake; akanaswa katika rima lao. Wakamtia katika tundu kwa kulabu, wakamleta kwa mfalme wa Babeli wakamtia ndani ya ngome, sauti yake isisikiwe tena juu ya milima ya Israeli. Mama yako alikuwa kama mzabibu, katika damu yako, uliopandwa karibu na maji; akazaa sana na kujaa matawi, kwa sababu ya maji mengi. Naye alikuwa na vijiti vya nguvu, kwa fimbo za enzi zao watawalao, na kimo chao kiliinuka kati ya matawi manene, wakaonekana kwa urefu wao, pamoja na wingi wa matawi yao. Lakini aling'olewa kwa ghadhabu, akaangushwa chini, upepo wa mashariki ukakausha matunda yake; vijiti vyake vya nguvu vikavunjika, vikakauka; moto ulivila. Na sasa umepandwa jangwani, katika nchi kavu, ya ukame. Na moto umetoka katika vijiti vya matawi yake, umekula matunda yake, hata hana tena kijiti cha nguvu kifaacho kwa fimbo ya enzi ya kutawala. Na hayo ni maombolezo, nayo yatakuwa maombolezo.
Ezekieli 19:1-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tena uwaombolezee wakuu wa Israeli, useme, Mama yako alikuwa nini? Simba mke; alijilaza kati ya simba, kati ya wana-simba aliwalisha watoto wake. Akamlea mtoto mmoja katika watoto wake, akawa mwana-simba, akajifunza kuwinda mawindo, akala watu. Mataifa nao wakapata habari zake, akanaswa katika rima lao, wakamchukua kwa kulabu mpaka nchi ya Misri. Basi mamaye alipoona kwamba amemngoja, na tumaini lake limepotea, akatwaa mtoto mwingine katika watoto wake, akamfanya mwana-simba. Naye akaenda huko na huko kati ya simba, akawa mwana-simba, akajifunza kuwinda mawindo, akala watu. Akayajua majumba yao, akaiharibu miji yao; nchi ikawa ukiwa, navyo vitu vilivyoijaza, kwa sababu ya mshindo wa kunguruma kwake. Ndipo mataifa wakajipanga juu yake pande zote toka nchi zote; wakaunda wavu wao juu yake; akanaswa katika rima lao. Wakamtia katika tundu kwa kulabu, wakamleta kwa mfalme wa Babeli wakamtia ndani ya ngome, sauti yake isisikiwe tena juu ya milima ya Israeli. Mama yako alikuwa kama mzabibu, katika damu yako, uliopandwa karibu na maji; akazaa sana na kujaa matawi, kwa sababu ya maji mengi. Naye alikuwa na vijiti vya nguvu, kwa fimbo za enzi zao watawalao, na kimo chao kiliinuka kati ya matawi manene, wakaonekana kwa urefu wao, pamoja na wingi wa matawi yao. Lakini aling’olewa kwa ghadhabu, akaangushwa chini, upepo wa mashariki ukakausha matunda yake; vijiti vyake vya nguvu vikavunjika, vikakauka; moto ulivila. Na sasa umepandwa jangwani, katika nchi kavu, ya ukame. Na moto umetoka katika vijiti vya matawi yake, umekula matunda yake, hata hana tena kijiti cha nguvu kifaacho kwa fimbo ya enzi ya kutawala. Na hayo ni maombolezo, nayo yatakuwa maombolezo.
Ezekieli 19:1-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Mungu aliniambia niimbe utenzi huu wa maombolezo kuhusu wakuu wa Israeli: Mama yenu alikuwa simba wa fahari miongoni mwa simba wengine. Alikaa kati ya simba vijana, akawalisha watoto wake. Alimlea mtoto mmojawapo wa watoto wake, mtoto huyo naye akawa simba kijana hodari. Akajifunza kwa mama yake kuwinda, akawa simba mla watu. Mataifa yakapiga mbiu ya hatari dhidi yake, wakamnasa katika mtego wao, wakampeleka kwa ndoana mpaka Misri. Mama yake alipoona kuwa amechoka kungoja, matumaini ya kumpata yamekwisha, alimchukua mtoto wake mwingine, akamfanya simba kijana hodari. Huyo alipokuwa amekua, akaanza kuzurura na simba wengine. Naye pia akajifunza kuwinda, akawa simba mla watu. Aliziandama ngome za watu na kuiharibu miji yao. Nchi ikatishika pamoja na wakazi wake, kwa sauti ya kunguruma kwake. Mataifa yakamkabili kutoka mkoani mwao kote, wakatandaza wavu wao juu yake, naye akanaswa katika mtego wao. Kwa ndoana wakamtia katika kizimba chao, wakampeleka kwa mfalme wa Babuloni. Huko, wakamtia gerezani, ili ngurumo yake isisikike tena juu ya milima ya Israeli. Mama yako alikuwa kama mzabibu shambani, uliopandikizwa kando ya maji, ambao ulizaa sana kwa kuwa na maji tele. Ulikuwa na matawi yenye nguvu, ambayo yalikuwa fimbo za kifalme. Mzabibu huo ulikua kupita miti mingine, watu waliusifu ukubwa wa shina lake na wingi wa matawi yake. Lakini ulingolewa kwa hasira ukatupwa chini ardhini; upepo wa mashariki ukaukausha, matunda yake yakapukutika; matawi yake yenye nguvu yalikaushwa, nao moto ukauteketeza. Na sasa umepandikizwa jangwani, katika nchi kame isiyo na maji. Lakini moto umetoka kwenye shina lake, umeyateketeza matawi na matunda yake. Matawi yake kamwe hayatakuwa na nguvu, wala hayatakuwa fimbo za kifalme. Huo umekuwa wimbo wa maombolezo; ndivyo unavyoimbwa daima.
Ezekieli 19:1-14 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Wewe fanya maombolezo kuhusu wakuu wa Israeli na useme: “ ‘Tazama jinsi gani mama yako alivyokuwa simba jike miongoni mwa simba! Alilala katikati ya wana simba na kulisha watoto wake. Alimlea mmoja wa watoto wake, naye akawa simba mwenye nguvu. Akajifunza kurarua mawindo naye akala watu. Mataifa wakasikia habari zake, naye akanaswa katika shimo lao. Wakamwongoza kwa ndoana mpaka nchi ya Misri. “ ‘Mama yake alipongoja na kuona tumaini lake halitimiziki, nayo matarajio yake yametoweka, akamchukua mwanawe mwingine na kumfanya simba mwenye nguvu. Alizungukazunguka miongoni mwa simba, kwa kuwa sasa alikuwa simba mwenye nguvu. Akajifunza kurarua mawindo naye akala watu. Akabomoa ngome zao na kuiharibu miji yao. Nchi na wote waliokuwa ndani yake wakatiwa hofu kwa kunguruma kwake. Kisha mataifa wakaja dhidi yake kutoka sehemu zilizomzunguka. Wakatanda nyavu zao kwa ajili yake, naye akanaswa katika shimo lao. Kwa kutumia ndoana wakamvutia kwenye tundu na kumleta mpaka kwa mfalme wa Babeli. Wakamtia gerezani, hivyo kunguruma kwake hakukusikika tena katika milima ya Israeli. “ ‘Mama yako alikuwa kama mzabibu katika shamba lako la mizabibu uliopandwa kando ya maji, ukiwa unazaa sana na wenye matawi mengi kwa sababu ya wingi wa maji. Matawi yake yalikuwa na nguvu, yaliyofaa kuwa fimbo ya enzi ya mtawala. Ulikuwa mrefu kupita miti mingine katikati ya matawi manene; ulionekana kwa urahisi kwa ajili ya urefu wake na wingi wa matawi yake. Lakini ulingʼolewa kwa hasira kali na kutupwa chini. Upepo wa mashariki uliufanya usinyae, matunda yake yakapukutika, matawi yake yenye nguvu yakanyauka na moto ukayateketeza. Sasa umepandwa jangwani katika nchi kame na ya kiu. Moto ulienea kuanzia katika mmojawapo ya matawi yake makubwa na kuteketeza matunda yake. Hakuna tawi lenye nguvu lililobaki juu yake lifaalo kuwa fimbo ya enzi ya mtawala.’ Hili ndilo ombolezo, na litumike kama ombolezo.”