Ezekieli 5:11
Ezekieli 5:11 Biblia Habari Njema (BHN)
Kwa sababu hiyo, kama niishivyo mimi Bwana Mwenyezi-Mungu, kwa vile mmeitia unajisi maskani yangu kwa machukizo yenu, mimi nitawakatilia mbali bila huruma na bila kumwacha mtu yeyote.
Ezekieli 5:11 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kwa hiyo hakika kama niishivyo, asema BWANA Mwenyezi, kwa kuwa mmenajisi mahali pangu patakatifu kwa sanamu zenu mbaya sana na desturi zenu za machukizo, mimi mwenyewe nitaondoa fadhili zangu kwenu.
Ezekieli 5:11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa sababu hiyo, kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hakika kwa kuwa umepatia unajisi patakatifu pangu, kwa matendo yako yote niyachukiayo, na kwa machukizo yako yote, kwa sababu hiyo mimi nami nitakupunguza; wala jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma.
Ezekieli 5:11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)