Mwanzo 47:5-6
Mwanzo 47:5-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Farao akamwambia Yosefu, “Baba yako na ndugu zako wamekujia wewe. Nchi yote ya Misri iko chini yako; wape baba yako na ndugu zako sehemu bora ya nchi hii. Waache wakae katika eneo la Gosheni. Na iwapo unawafahamu watu stadi miongoni mwao, wateue wawe waangalizi wa mifugo yangu.”
Mwanzo 47:5-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Farao akamwambia Yusufu, akisema, Baba yako na ndugu zako wamekujia; nchi ya Misri iko mbele yako, palipo pema pa nchi uwakalishe baba yako na ndugu zako; na wakae katika nchi ya Gosheni. Tena ukijua ya kuwa wako watu hodari miongoni mwao, uwaweke wawe wakuu wa wanyama wangu.
Mwanzo 47:5-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Farao akamwambia Yusufu, akisema, Baba yako na ndugu zako wamekujia; nchi ya Misri iko mbele yako, palipo pema pa nchi uwakalishe baba yako na ndugu zako; na wakae katika nchi ya Gosheni. Tena ukijua ya kuwa wako watu hodari miongoni mwao, uwaweke wawe wakuu wa wanyama wangu.
Mwanzo 47:5-6 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Farao akamwambia Yosefu, “Baba yako na ndugu zako wamekuja kwako, nayo nchi ya Misri ipo mbele yako, uwakalishe baba yako na ndugu zako katika sehemu iliyo bora kupita zote katika nchi. Na waishi Gosheni. Kama unamfahamu yeyote miongoni mwao mwenye uwezo maalum, waweke wawe wasimamizi wa mifugo yangu.”