Mwanzo 49:3-4
Mwanzo 49:3-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza, Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu. Umeruka mpaka kama maji, basi usiwe na ukuu, Kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako, Ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu.
Mwanzo 49:3-4 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Reubeni, wewe ni mzaliwa wangu wa kwanza, nguvu zangu, tunda la kwanza la nguvu zangu, umepita kwa heshima, umepita kwa uwezo. Usiyezuiwa kama maji, basi hutakuwa mkuu tena, kwa kuwa ulipanda kwenye kitanda cha baba yako, kwenye kitanda changu na kukinajisi.
Mwanzo 49:3-4 Biblia Habari Njema (BHN)
“Wewe Reubeni ni mzaliwa wangu wa kwanza, nguvu yangu na tunda la ujana wangu. Wewe wawapita ndugu zako kwa ukuu na nguvu. “Wewe ni kama maji ya mafuriko. Lakini hutakuwa wa kwanza tena, maana ulipanda kitandani mwangu mimi baba yako, wewe ulikitia najisi; naam wewe ulikipanda!
Mwanzo 49:3-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza, Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu. Umekuwa kama maji yavukavyo mpaka, basi nawe hutafana tena, Kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako, Ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu.