Mwanzo 5:18-32
Mwanzo 5:18-32 Biblia Habari Njema (BHN)
Yaredi alipokuwa na umri wa miaka 162, alimzaa Henoki. Baada ya kumzaa Henoki, Yaredi aliishi miaka 800 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Yaredi alifariki akiwa na umri wa miaka 962. Henoki alipokuwa na umri wa miaka 65, alimzaa Methusela. Henoki alikuwa mcha Mungu. Baada ya kumzaa Methusela, Henoki aliishi miaka 300 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Henoki aliishi miaka 365. Alikuwa mcha Mungu, akatoweka, kwa maana Mungu alimchukua. Wakati Methusela alipokuwa na umri wa miaka 187, alimzaa Lameki. Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka 782, na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Methusela alifariki akiwa na umri wa miaka 969. Wakati Lameki alipokuwa na umri wa miaka 182, alimzaa mtoto wa kiume. Alimwita mtoto huyo Noa, akisema, “Mtoto huyu ndiye atakayetufariji kutokana na kazi yetu ngumu tunayofanya kwa mikono yetu katika ardhi aliyoilaani Mwenyezi-Mungu.” Baada ya kumzaa Noa, Lameki aliishi miaka 595 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. Lameki alifariki akiwa na umri wa miaka 777. Noa alipokuwa na umri wa miaka 500, alimzaa Shemu na Hamu na Yafethi.
Mwanzo 5:18-32 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Yaredi akaishi miaka mia moja na sitini na miwili, akamzaa Henoko. Yaredi akaishi baada ya kumzaa Henoko miaka mia nane, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Siku zote za Yaredi ni miaka mia tisa na sitini na miwili, akafa. Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela. Henoko akaenda pamoja na Mungu. Baada ya kumzaa Methusela aliishi miaka mia tatu, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano. Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa. Methusela akaishi miaka mia moja na themanini na saba, akamzaa Lameki. Methusela akaishi baada ya kumzaa Lameki miaka mia saba na themanini na miwili, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Siku zote za Methusela ni miaka mia tisa na sitini na tisa, akafa. Lameki akaishi miaka mia moja na themanini na miwili, akazaa mwana. Akamwita jina lake Nuhu, akinena, Huyu ndiye atakayetufariji kwa kazi yetu na kwa taabu ya mikono yetu katika nchi aliyoilaani BWANA. Lameki akaishi baada ya kumzaa Nuhu miaka mia tano na tisini na mitano, akazaa wana, wa kiume na wa kike. Siku zote za Lameki ni miaka mia saba na sabini na saba, akafa. Baada ya Nuhu kufikisha umri wa miaka mia tano, aliwazaa Shemu, na Hamu, na Yafethi.
Mwanzo 5:18-32 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Yaredi akaishi miaka mia na sitini na miwili, akamzaa Henoko. Yaredi akaishi baada ya kumzaa Henoko miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake. Siku zote za Yaredi ni miaka mia kenda na sitini na miwili, akafa. Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela. Henoko akaenda pamoja na Mungu baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana, waume na wake. Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano. Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa. Methusela akaishi miaka mia na themanini na saba, akamzaa Lameki. Methusela akaishi baada ya kumzaa Lameki miaka mia saba na themanini na miwili, akazaa wana, waume na wake. Siku zote za Methusela ni miaka mia kenda na sitini na kenda, akafa. Lameki akaishi miaka mia na themanini na miwili, akazaa mwana. Akamwita jina lake Nuhu, akinena, Huyu ndiye atakayetufariji kwa kazi yetu na kwa taabu ya mikono yetu katika nchi aliyoilaani BWANA. Lameki akaishi baada ya kumzaa Nuhu miaka mia na tisini na mitano, akazaa wana, waume na wake. Siku zote za Lameki ni miaka mia saba na sabini na saba, akafa. Nuhu alikuwa mwenye miaka mia tano, Nuhu akawazaa Shemu, na Hamu, na Yafethi.
Mwanzo 5:18-32 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Yaredi alipokuwa ameishi miaka mia moja na sitini na mbili (162), akamzaa Idrisi. Baada ya kumzaa Idrisi, Yaredi aliishi miaka mia nane, naye akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. Yaredi aliishi jumla ya miaka mia tisa na sitini na mbili (962), ndipo akafa. Idrisi alipokuwa ameishi miaka sitini na tano, akamzaa Methusela. Baada ya kumzaa Methusela, Idrisi alitembea na Mungu miaka mia tatu, na akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. Idrisi aliishi jumla ya miaka mia tatu sitini na tano (365). Idrisi akatembea na Mungu, kisha akatoweka, kwa sababu Mungu alimchukua. Methusela alipokuwa ameishi miaka mia moja na themanini na saba (187), akamzaa Lameki. Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka mia saba na themanini na mbili (782), akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. Methusela aliishi jumla ya miaka mia tisa sitini na tisa (969), ndipo akafa. Lameki alipokuwa ameishi miaka mia moja na themanini na mbili (182), alimzaa mwana. Akamwita jina Nuhu. Naye akasema, “Huyu ndiye atakayetufariji katika kazi ngumu ya mikono yetu yenye maumivu makali yaliyosababishwa na ardhi iliyolaaniwa na Mwenyezi Mungu.” Baada ya Nuhu kuzaliwa, Lameki aliishi miaka mia tano na tisini na tano (595), akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. Lameki aliishi jumla ya miaka mia saba sabini na saba (777), ndipo akafa. Baada ya Nuhu kuishi miaka mia tano, aliwazaa Shemu, Hamu, na Yafethi.