Waebrania 7:22-25
Waebrania 7:22-25 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kwa ajili ya kiapo hiki, Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi. Basi pamekuwepo na makuhani wengi wa aina hiyo, kwa kuwa kifo kiliwazuia kuendelea na huduma yao ya ukuhani. Lakini kwa sababu Yesu anaishi milele, anao ukuhani wa kudumu. Kwa hiyo anaweza kuwaokoa kabisa wale wanaomjia Mungu kupitia kwake, kwa sababu yeye adumu daima kuomba kwa ajili yao.
Waebrania 7:22-25 Biblia Habari Njema (BHN)
Basi, kutokana na tofauti hii, Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi. Tena: Hao makuhani wengine walikuwa wengi kwa sababu walikufa na hawakuweza kuendelea na kazi yao. Lakini Yesu si kama wao, yeye anaishi milele; ukuhani wake hauondoki kwake. Hivyo, yeye anaweza daima kuwaokoa kabisa wote wanaomwendea Mungu kwa njia yake, maana yeye anaishi milele kuwaombea kwa Mungu.
Waebrania 7:22-25 Swahili Revised Union Version (SRUV)
basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi. Tena wale walifanywa makuhani wengi, kwa sababu walizuiliwa na mauti wasikae; bali yeye, kwa kuwa anakaa milele, anao ukuhani wake usioondoka. Naye, kwa sababu hii, anaweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.
Waebrania 7:22-25 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi. Tena wale walifanywa makuhani wengi, kwa sababu wazuiliwa na mauti wasikae; bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka. Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.