Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 19:1-15

Isaya 19:1-15 Biblia Habari Njema (BHN)

Kauli ya Mungu dhidi ya nchi ya Misri. “Mwenyezi-Mungu amepanda juu ya wingu liendalo kasi na kuja mpaka nchi ya Misri. Sanamu za miungu ya Wamisri zitatetemeka mbele yake, mioyo ya Wamisri itayeyuka kwa hofu. Mimi nitawachochea Wamisri wagongane: Ndugu na ndugu yake, jirani na jirani yake, mji mmoja na mji mwingine, mfalme mmoja na mfalme mwingine. Nitawaondolea Wamisri uhodari wao, nitaivuruga mipango yao; watatafuta maoni kwa sanamu na mizimu, wachawi, mizuka na pepo. Nitawatia Wamisri mikononi mwa bwana katili, mfalme mkali ambaye atawatawala. Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshi, nimenena.” Maji ya mto Nili yatakaushwa, nao utakauka kabisa. Mifereji yake itatoa uvundo, vijito vyake vitapunguka na kukauka. Nyasi na mafunjo yake yataoza. Sehemu za kandokando ya Nili zitakuwa tupu. Mimea yote iliyopandwa humo itakauka na kupeperushiwa mbali na kutoweka. Wavuvi watalia na kuomboleza, wote watumiao ndoana watalalama; wote wanaotanda nyavu majini watakufa moyo. Wafuma nguo za kitani watakata tamaa, wote kwa pamoja watakufa moyo. Wafuma nguo watafedheheshwa, na vibarua watahuzunika. Viongozi wa mji wa Soani ni wapumbavu kabisa, washauri wa Farao wanatoa shauri la kijinga! Awezaje kila mmoja kumwambia Farao, “Mimi ni mzawa wa mtaalamu stadi; mzawa wa wafalme wa hapo kale!” Wako wapi, ewe Farao, wataalamu wako? Waache basi wakuambie na kukujulisha aliyopanga Mwenyezi-Mungu wa majeshi dhidi ya Misri! Lakini viongozi wa Soani ni wapumbavu, wakuu wa Memfisi wamedanganyika. Hao walio msingi wa makabila yao wamelipotosha taifa la Misri. Mwenyezi-Mungu amewamwagia hali ya vurugu, wakawapotosha Wamisri katika mipango yao yote, wakawa kama mlevi anayeyumbayumba akitapika. Hakuna mtu yeyote nchini Misri, kiongozi au raia, mashuhuri au duni, awezaye kufanya lolote la maana.

Shirikisha
Soma Isaya 19

Isaya 19:1-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Ufunuo juu ya Misri. Tazama, BWANA amepanda juu ya wingu jepesi, anafika Misri; na sanamu za Misri zinatikisika mbele zake, na moyo wa Misri unayeyuka ndani yake. Nami nitawaamsha Wamisri juu ya Wamisri; nao watapigana, kila mtu na ndugu yake, na kila mtu na jirani yake, mji juu ya mji, na ufalme juu ya ufalme. Na roho yao Misri itaondolewa, nami nitaiharibu mipango yao, nao watakwenda kwa sanamu zao, na kwa waganga, na kwa wapiga ramli na kwa wachawi. Nami nitawatoa hao Wamisri na kuwatia katika mikono ya bwana mgumu; na mfalme mkali atawatawala; asema Bwana, BWANA wa majeshi. Na maji ya baharini yatapunguka, na huo mto utakauka na kuwa pakavu. Na vijito vya mto vitatoa uvundo, na mifereji ya Misri itakuwa haina maji mengi, itakauka; manyasi na mianzi itanyauka. Vitu vimeavyo karibu na Nile, katika ukingo wa Nile, na vyote vilivyopandwa karibu na Nile vitakauka na kuondolewa na kutoweka. Na wavuvi wataugua, na wote wavuao kwa ndoana watahuzunika, nao watandao jarife juu ya maji watazimia. Tena wao wafanyao kazi ya kuchana kitani watafadhaika, na hao pia wafumao bafta. Na nguzo za nchi zitavunjika vipande vipande, wote wafanyao kazi ya mshahara watahuzunika nafsini mwao. Wakuu wa Soani wamekuwa wapumbavu kabisa; washauri wenye hekima wa Farao, ushauri wao umepumbazika; mwawezaje kumwambia Farao, Mimi ni mwana wa wenye hekima, ni mwana wa wafalme wa zamani? Wako wapi, basi, watu wako wenye hekima? Na wakuambie sasa; na wajue mambo aliyokusudia BWANA wa majeshi juu ya Misri. Wakuu wa Soani wamekuwa wapumbavu, wakuu wa Nofu wamedanganyika; na hao walio mawe ya pembeni ya kabila zake wameipotosha Misri. Yeye BWANA ametia roho ya ushupavu katika moyo wa Misri, nao wameikosesha Misri katika matendo yake yote, kama mlevi aendavyo huku na huko akitapika. Wala haitakuwako kazi yoyote katika Misri iwezayo kufanywa, ya kichwa au ya mkia, ya tawi au ya nyasi.

Shirikisha
Soma Isaya 19

Isaya 19:1-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Ufunuo juu ya Misri. Tazama, BWANA amepanda juu ya wingu jepesi, anafika Misri; na sanamu za Misri zinatikisika mbele zake, na moyo wa Misri unayeyuka ndani yake. Nami nitawaamsha Wamisri juu ya Wamisri; nao watapigana, kila mtu na ndugu yake, na kila mtu na jirani yake, mji juu ya mji, na ufalme juu ya ufalme. Na roho ya Misri itamwagika kabisa katikati yake, nami nitayabatilisha mashauri yake, nao watakwenda kwa sanamu zao, na kwa waganga, na kwa wapiga ramli, na kwa wachawi. Nami nitawatoa hao Wamisri na kuwatia katika mikono ya bwana mgumu; na mfalme mkali atawatawala; asema Bwana, BWANA wa majeshi. Na maji ya baharini yatapunguka, na huo mto utakauka na kuwa pakavu. Na vijito vya mto vitatoa uvundo, na mifereji ya Misri itakuwa haina maji mengi, itakauka; manyasi na mianzi itanyauka. Vitu vimeavyo karibu na Nile, katika ukingo wa Nile, na vyote vilivyopandwa karibu na Nile vitakauka na kuondolewa na kutoweka. Na wavuvi wataugua, na wote wavuao kwa ndoana watahuzunika, nao watandao jarife juu ya maji watazimia. Tena wao wafanyao kazi ya kuchana kitani watafadhaika, na hao pia wafumao bafta. Na nguzo za nchi zitavunjika vipande vipande, wote wafanyao kazi ya mshahara watahuzunika nafsini mwao. Wakuu wa Soani wamekuwa wapumbavu kabisa; washauri wenye hekima wa Farao, shauri lao limepumbazika; mwawezaje kumwambia Farao, Mimi ni mwana wa wenye hekima, ni mwana wa wafalme wa zamani? Wako wapi, basi, watu wako wenye hekima? Na wakuambie sasa; na wajue mambo aliyokusudia BWANA wa majeshi juu ya Misri. Wakuu wa Soani wamekuwa wapumbavu, wakuu wa Nofu wamedanganyika; na hao walio mawe ya pembeni ya kabila zake wameikosesha Misri. Yeye BWANA ametia roho ya ushupavu katika moyo wa Misri, nao wameikosesha Misri katika matendo yake yote, kama mlevi aendavyo huko na huko akitapika. Wala haitakuwako kazi yo yote katika Misri iwezayo kufanywa, ya kichwa au ya mkia, ya tawi au ya nyasi.

Shirikisha
Soma Isaya 19

Isaya 19:1-15 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

Neno la unabii kuhusu Misri: Tazama, BWANA amepanda juu ya wingu liendalo kwa haraka naye anakuja Misri. Sanamu za Misri zinatetemeka mbele yake, nayo mioyo ya Wamisri inayeyuka ndani yao. “Nitamchochea Mmisri dhidi ya Mmisri, ndugu atapigana dhidi ya ndugu, jirani dhidi ya jirani, mji dhidi ya mji, ufalme dhidi ya ufalme. Wamisri watakufa moyo, na nitaibatilisha mipango yao. Watatafuta ushauri kwa sanamu na kwa roho za waliokufa, kwa waaguzi na kwa wale waongeao na mizimu. Nitawatia Wamisri mikononi mwa bwana mkatili na mfalme mkali atawatawala,” asema Bwana, BWANA wa majeshi. Maji ya mito yatakauka, chini ya mto kutakauka kwa jua. Mifereji itanuka; vijito vya Misri vitapungua na kukauka. Matete na nyasi vitanyauka, pia mimea iliyo kando ya Mto Naili, pale mto unapomwaga maji baharini. Kila shamba lililopandwa kando ya Mto Naili litakauka, litapeperushwa na kutoweka kabisa. Wavuvi watalia na kuomboleza, wote watupao ndoana katika Mto Naili, na watupao nyavu katika maji watadhoofika kwa majonzi. Wale watu wafanyao kazi ya kitani kilichochambuliwa watakata tamaa, wafumaji wa kitani safi watavunjika moyo. Wafanyao kazi ya kufuma nguo watahuzunishwa, nao vibarua wataugua moyoni. Maafisa wa Soani ni wapumbavu kabisa, washauri wa Farao wenye busara wanatoa ushauri wa kijinga. Unawezaje kumwambia Farao, “Mimi ni mmoja wa watu wenye hekima, mwanafunzi wa wafalme wa zamani”? Wako wapi sasa watu wako wenye hekima? Wao wakuoneshe na kukufahamisha ni nini BWANA wa majeshi amepanga dhidi ya Misri. Maafisa wa Soani wamekuwa wapumbavu, viongozi wa Memfisi wamedanganyika, walio mawe ya pembe ya taifa lake wameipotosha Misri. BWANA amewamwagia roho ya kizunguzungu; wanaifanya Misri iyumbayumbe katika yale yote inayoyafanya, kama vile mlevi ayumbayumbavyo katika kutapika kwake. Misri haiwezi kufanya kitu chochote, cha kichwa wala cha mkia, cha tawi la mtende wala cha tete.

Shirikisha
Soma Isaya 19