Isaya 22:1-14
Isaya 22:1-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Kauli ya Mungu dhidi ya Bonde la Maono. Kuna nini ee Yerusalemu? Mbona watu wote mmepanda juu ya nyumba? Kwa nini mnapiga kelele za shangwe, na mji wote umechangamka na kujaa vigelegele? Watu wenu waliokufa hawakuuawa vitani, wala hawakuuawa katika mapigano. Maofisa wenu wote walikimbia, wakakamatwa hata kabla ya kufyatua mshale mmoja. Watu wako wote waliopatikana walitekwa, ingawa walikuwa wamekimbilia mbali. Ndiyo maana nawaambieni: Msijali chochote juu yangu niacheni nilie machozi ya uchungu. Msijisumbue kunifariji kwa ajili ya balaa walilopata watu wangu. Maana leo Mwenyezi-Mungu wa majeshi ametuletea mchafuko: Kushindwa na wasiwasi katika Bonde la Maono. Kuta za mji zimebomolewa, mayowe ya wakazi wake yasikika mpaka milimani. Majeshi ya Elamu, pinde na mishale mikononi, walikuja wamepanda farasi na magari ya vita; nalo jeshi la Kiri lilitayarisha ngao zake. Mabonde yako mazuri ewe Yerusalemu, yalijaa magari ya vita na farasi; wapandafarasi walijipanga tayari langoni mwako. Ulinzi wote wa Yuda uliporomoka. Siku hiyo mlikwenda kutafuta silaha zilizokuwa zimehifadhiwa katika Nyumba ya Msitu, mkaona kwamba nyufa za kuta za mji wa Daudi ni nyingi, mkajaza maji bwawa la chini. Mlizikagua nyumba za mji wa Yerusalemu, mkabomoa baadhi yake ili kupata mawe ya kuimarisha kuta za mji. Katikati ya kuta hizo mlijijengea birika la kuhifadhia maji yanapotiririka kutoka bwawa la zamani. Lakini hamkumtafuta Mungu aliyepanga mambo haya yote; hamkumjali yeye aliyepanga hayo yote tangu zamani. Siku hiyo, Mwenyezi-Mungu, wa majeshi aliwataka mlie na kuomboleza, mnyoe nywele na kuvaa mavazi ya gunia. Lakini nyinyi mkafurahi na kusherehekea. Mlichinja ng'ombe na kondoo, mkala nyama na kunywa divai. Nyinyi mlisema: “Acha tule na kunywa maana kesho tutakufa.” Mwenyezi-Mungu wa majeshi alinifunulia haya akisema: “Hakika hawatasamehewa uovu huu, watakufa bila kusamehewa. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.”
Isaya 22:1-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ufunuo juu ya bonde la maono. Sasa una nini, wewe, Hata umepanda pia juu ya madari ya nyumba? Ewe uliyejaa makelele, Mji wa ghasia, mji wenye furaha; Watu wako waliouawa hawakuuawa kwa upanga, Wala hawakufa vitani. Wakuu wako wote wamekimbia pamoja, Wamefungwa wasiutumie upinde. Wote walioonekana wamefungwa pamoja, Wamekimbia mbali sana. Kwa sababu hiyo nasema, Geuza uso wako usinitazame, nipate kulia kwa uchungu; usijishughulishe kunifariji, kwa ajili ya kuharibika kwake binti ya watu wangu. Kwa maana siku ya kutaabika, siku ya kukanyagwa, siku ya fujo inakuja, itokayo kwa Bwana, BWANA wa majeshi, katika bonde la Maono; inabomoa kuta; na kuililia milima. Na Elamu wameshika podo, pamoja na magari ya vita, na watu wenye kupanda farasi; na Kiri wameifunua ngao. Hata ikawa mabonde yako mateule yamejaa magari ya vita, nao wapandao farasi wamejipanga katika malango. Kisha alikiondoa kifuniko cha Yuda, nawe siku hiyo ulivitazama vyombo vya vita katika nyumba ya mwituni. Nanyi mlipaona mahali palipobomoka katika mji wa Daudi ya kuwa ni pengi, nanyi mliyakusanya maji ya birika la chini. Nanyi mlizihesabu nyumba za Yerusalemu, mkazibomoa nyumba ili kuutia nguvu ukuta. Nanyi mlifanya birika la maji katikati ya kuta mbili, la kuwekea maji ya birika la kale; lakini hamkumwangalia yeye aliyeyafanya hayo, wala kumjali yeye aliyeyatengeneza zamani. Siku hiyo Bwana, BWANA wa majeshi, akawaita watu walie na kuomboleza, na kung'oa nywele zao, na kuvaa nguo za magunia; na kumbe! Furaha, na kuchekelea, na kuchinja ng'ombe, na kuchinja kondoo, na kula nyama, na kunywa mvinyo; tule, tunywe, kwa maana kesho tutakufa. Na yeye BWANA wa majeshi akafunua haya masikioni mwangu, Ni kweli, uovu huu hautatakaswa wala kuwatokeni hata mfe; asema Bwana, BWANA wa majeshi.
Isaya 22:1-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ufunuo juu ya bonde la maono. Sasa una nini, wewe, Hata umepanda pia juu ya dari za nyumba? Ewe uliyejaa makelele, Mji wa ghasia, mji wenye furaha; Watu wako waliouawa hawakuuawa kwa upanga, Wala hawakufa vitani. Wakuu wako wote wamekimbia pamoja, Wamefungwa wasiutumie upinde. Wote walioonekana wamefungwa pamoja, Wamekimbia mbali sana. Kwa sababu hiyo nasema, Geuza uso wako usinitazame, nipate kulia kwa uchungu; usijishughulishe kunifariji, kwa ajili ya kuharibika kwake binti ya watu wangu. Kwa maana siku ya kutaabika, siku ya kukanyagwa, siku ya fujo inakuja, itokayo kwa Bwana, BWANA wa majeshi, katika bonde la Maono; inabomoa kuta; na kuililia milima. Na Elamu wameshika podo, pamoja na magari ya vita, na watu wenye kupanda farasi; na Kiri wameifunua ngao. Hata ikawa mabonde yako mateule yamejaa magari ya vita, nao wapandao farasi wamejipanga wakielekea malango. Kisha alikiondoa kifuniko cha Yuda, nawe siku hiyo ulivitazama vyombo vya vita katika nyumba ya mwituni. Nanyi mlipaona mahali palipobomoka katika mji wa Daudi ya kuwa ni pengi, nanyi mliyakusanya maji ya birika la chini. Nanyi mlizihesabu nyumba za Yerusalemu, mkazibomoa nyumba ili kuutia nguvu ukuta. Nanyi mlifanya birika la maji katikati ya kuta mbili, la kuwekea maji ya birika la kale; lakini hamkumwangalia yeye aliyeyafanya hayo, wala kumjali yeye aliyeyatengeneza zamani. Siku hiyo Bwana, BWANA wa majeshi, akawaita watu walie na kuomboleza, na kung’oa nywele zao, na kuvaa nguo za magunia; na kumbe! Furaha, na kuchekelea, na kuchinja ng’ombe, na kuchinja kondoo, na kula nyama, na kunywa mvinyo; tule, tunywe, kwa maana kesho tutakufa. Na yeye BWANA wa majeshi akafunua haya masikioni mwangu, Ni kweli, uovu huu hautatakaswa wala kuwatokeni hata mfe; asema Bwana, BWANA wa majeshi.
Isaya 22:1-14 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Neno la unabii kuhusu Bonde la Maono: Nini kinachokutaabisha sasa, kwamba ninyi nyote mmepanda juu ya mapaa? Ewe mji uliojaa ghasia, ewe mji wa makelele na sherehe! Watu wenu waliokufa hawakuuawa kwa upanga, wala hawakufa vitani. Viongozi wako wote wamekimbia pamoja, wamekamatwa bila kutumia upinde. Ninyi nyote mliokamatwa mlichukuliwa wafungwa pamoja, mlikimbia wakati adui alipokuwa bado mbali. Kwa hiyo nilisema, “Geukia mbali nami, niache nilie kwa uchungu. Usijaribu kunifariji juu ya maangamizi ya watu wangu.” Bwana, BWANA wa majeshi, anayo siku ya ghasia, ya kukanyaga, na ya kuogofya katika Bonde la Maono, siku ya kuangusha kuta na ya kupiga kelele hadi milimani. Elamu analichukua podo, pamoja na waendesha magari ya vita na farasi. Kiri anaifungua ngao. Mabonde yako yaliyo mazuri sana yamejaa magari ya vita, nao wapanda farasi wamewekwa kwenye malango ya mji. Ulinzi wa Yuda umeondolewa. Nawe ulitazama siku ile silaha katika Jumba la Kifalme la Mwituni. Mkaona kuwa Mji wa Daudi una matundu mengi katika ulinzi wake, mkaweka akiba ya maji kwenye Bwawa la Chini. Mlihesabu majengo katika Yerusalemu nanyi mkabomoa nyumba ili kuimarisha ukuta. Mlijenga bwawa la maji katikati ya kuta mbili kwa ajili ya maji ya Bwawa la Zamani, lakini hamkumtazama Yule aliyelitengeneza, au kuwa na heshima kwa Yule aliyeubuni tangu zamani za kale. Bwana, BWANA wa majeshi, aliwaita siku ile ili kulia na kuomboleza, kungʼoa nywele zenu na kuvaa magunia. Lakini tazama, kuna furaha na sherehe, kuchinja ngʼombe na kuchinja kondoo, kula nyama na kunywa mvinyo! Mnasema, “Tuleni na kunywa, kwa kuwa kesho tutakufa!” BWANA wa majeshi amelifunua hili nikiwa ninasikia: Bwana, BWANA wa majeshi, asema: “Hadi siku ya kufa kwenu, dhambi hii haitafanyiwa upatanisho.”