Isaya 40:6-7
Isaya 40:6-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Sikiliza! Kuna sauti inasema, “Tangaza!” Nami nikauliza, “Nitangaze nini?” Naye: “Tangaza: Binadamu wote ni kama majani; uthabiti wao ni kama ua la shambani. Majani hunyauka na ua hufifia, Mwenyezi-Mungu avumishapo upepo juu yake. Hakika binadamu ni kama majani.
Isaya 40:6-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Sikiliza, ni sauti ya mtu asemaye, Lia! Nikasema, Nilie nini? Watu wote ni majani, Na wema wake wote ni kama ua la shambani; Majani yakauka, ua lanyauka; Kwa sababu pumzi ya BWANA yapita juu yake. Hakika watu ni majani.
Isaya 40:6-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Sikiliza, ni sauti ya mtu asemaye, Lia! Nikasema, Nilie nini? Wote wenye mwili ni majani, Na wema wake wote ni kama ua la kondeni; Majani yakauka, ua lanyauka; Kwa sababu pumzi ya BWANA yapita juu yake. Yakini watu hawa ni majani.
Isaya 40:6-7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Sauti husema, “Piga kelele.” Nami nikasema, “Nipige kelele gani?” “Wanadamu wote ni kama majani, nao utukufu wao wote ni kama maua ya kondeni. Majani hunyauka na maua huanguka, kwa sababu pumzi ya BWANA huyapuliza. Hakika wanadamu ni majani.