Isaya 48:17-18
Isaya 48:17-18 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu, Mtakatifu wa Israeli, Mkombozi wako, asema hivi: “Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ninayekufundisha kwa faida yako, ninayekuongoza katika njia unayotakiwa kwenda. Laiti ungalizitii amri zangu! Hapo baraka zingekutiririkia kama mto, ungepata fanaka kwa wingi kama mawimbi ya bahari.
Isaya 48:17-18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni BWANA, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata. Laiti ungalisikiliza amri zangu! Ndipo amani yako ingalikuwa kama mto wa maji, na haki yako kama mawimbi ya bahari
Isaya 48:17-18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni BWANA, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata. Laiti ungalisikiliza amri zangu! Ndipo amani yako ingalikuwa kama mto wa maji, na haki yako kama mawimbi ya bahari
Isaya 48:17-18 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Hili ndilo asemalo BWANA, Mkombozi wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli: “Mimi ni BWANA, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye katika njia ikupasayo kuiendea. Laiti ungesikiliza kwa makini maagizo yangu, amani yako ingekuwa kama mto, haki yako kama mawimbi ya bahari.