Nembo ya Programu ya Biblia
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 5:24 - Linganisha Matoleo Yote

Isaya 5:24 BHN (Biblia Habari Njema)

Kwa hiyo, kama moto uteketezavyo nyasi, kama majani yateketeavyo katika mwali wa moto ndivyo na mizizi yao itakavyooza, na maua yao yatakavyopeperushwa juu kama vumbi. Maana wameiacha sheria ya Mwenyezi-Mungu wa majeshi, wamedharau neno la yule Mtakatifu wa Israeli.

Shirikisha
Isaya 5 BHN

Isaya 5:24 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Kwa hiyo kama vile mwali wa moto uteketezavyo mabua makavu, na kama manyasi makavu yaangukavyo katika mwali wa moto; kadhalika shina lao litakuwa kama ubovu, na ua lao litapeperushwa juu kama mavumbi; kwa sababu wameikataa sheria ya BWANA wa majeshi, na kulidharau neno lake aliye Mtakatifu wa Israeli.

Shirikisha
Isaya 5 SUV

Isaya 5:24 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Kwa hiyo kama vile muali wa moto uteketezavyo mabua makavu, na kama manyasi makavu yaangukavyo katika muali wa moto; kadhalika shina lao litakuwa kama ubovu, na ua lao litapeperushwa juu kama mavumbi; kwa sababu wameikataa sheria ya BWANA wa majeshi, na kulidharau neno lake aliye Mtakatifu wa Israeli.

Shirikisha
Isaya 5 SRUV

Isaya 5:24 NEN (Neno)

Kwa hiyo, kama ndimi za moto zinavyoteketeza nyasi, na kama vile majani makavu yanavyozama katika miali ya moto, ndivyo mizizi yao itakavyooza, na maua yao yatakavyopeperushwa kama mavumbi; kwa kuwa wameikataa sheria ya BWANA wa majeshi na kulisukumia mbali neno la Aliye Mtakatifu wa Israeli.

Shirikisha
Isaya 5 NEN