Isaya 65:20
Isaya 65:20 Biblia Habari Njema (BHN)
Hakutakuwa tena na vifo vya watoto wachanga, wazee nao hawatakufa kabla ya wakati wao. Akifa mtu wa miaka 100 amekufa akiwa kijana; na akifa kabla ya miaka 100 ni balaa.
Isaya 65:20 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hatakuwapo tena mtoto wa siku chache, wala mzee asiyetimia siku zake; kwa maana mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia; bali mtenda dhambi mwenye umri wa miaka mia atalaaniwa.
Isaya 65:20 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hatakuwapo tena mtoto wa siku chache, wala mzee asiyetimia siku zake; kwa maana mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia; bali mtenda dhambi mwenye umri wa miaka mia atalaaniwa.
Isaya 65:20 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Kamwe hatakuwepo tena ndani yake mtoto mchanga atakayeishi siku chache tu, au mzee ambaye hataishi akatimiza miaka yake. Yeye atakayekufa akiwa na umri wa miaka mia moja atahesabiwa kwamba ni kijana tu, yeye ambaye hatafika miaka mia moja, atahesabiwa kuwa amelaaniwa.