Yeremia 21:8-9
Yeremia 21:8-9 Biblia Habari Njema (BHN)
“Nawe Yeremia utawaambia watu hawa kwamba mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Sikilizeni! Mimi nawapeni nafasi ya kuchagua njia ya uhai au njia ya kifo. Mtu atakayebaki mjini humu atauawa kwa upanga au kwa njaa au kwa maradhi mabaya. Lakini mtu atakayetoka nje ya mji na kujisalimisha kwa Wakaldayo wanaouzingira mji, ataishi; naam, atayanusurisha maisha yake.
Yeremia 21:8-9 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Zaidi ya hayo, waambie watu hawa, ‘Hili ndilo asemalo BWANA: Tazama, naweka mbele yenu njia ya uzima, na njia ya mauti. Yeyote atakayekaa katika mji huu atakufa kwa upanga, njaa au tauni. Lakini yeyote atakayetoka na kujisalimisha kwa Wakaldayo ambao wameuzunguka mji huu kwa jeshi, atanusurika, naye ataishi.
Yeremia 21:8-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nawe waambie watu hawa, BWANA asema hivi, Tazama naweka mbele yenu njia ya uzima, na njia ya mauti. Yeye atakayekaa katika mji huu atakufa kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni; bali yeye atakayetoka, na kujitia pamoja na Wakaldayo wanaowahusuru, yeye ataishi, na maisha yake yatakuwa nyara kwake.
Yeremia 21:8-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)