Yeremia 3:13-14
Yeremia 3:13-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Wewe, kiri tu kosa lako: Kwamba umeniasi mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako; kwamba chini ya kila mti wenye majani, umewapa miungu wengine mapenzi yako wala hukuitii sauti yangu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. “Rudini, enyi watoto msio na uaminifu, maana, mimi ndimi Bwana wenu. Nitawachukua mmoja kutoka kila mji, na wawili kutoka katika kila ukoo, niwapeleke hadi mlimani Siyoni. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Yeremia 3:13-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ungama uovu wako tu; ya kwamba umemwasi BWANA, Mungu wako, na njia zako zimekuwa nyingi kuwaendea wageni chini ya kila mti wenye majani mabichi, wala hamkuitii sauti yangu, asema BWANA. Rudini, enyi watoto wenye kuasi, asema BWANA; maana mimi ni mume wenu; nami nitatwaa mtu mmoja wa mji mmoja, na wawili wa jamaa moja, nami nitawaleta hadi Sayuni
Yeremia 3:13-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ungama uovu wako tu; ya kwamba umemwasi BWANA, Mungu wako, na njia zako zimekuwa nyingi kuwaendea wageni chini ya kila mti wenye majani mabichi, wala hamkuitii sauti yangu, asema BWANA. Rudini, enyi watoto wenye kuasi, asema BWANA; maana mimi ni mume wenu; nami nitatwaa mtu mmoja wa mji mmoja, na wawili wa jamaa moja, nami nitawaleta hata Sayuni
Yeremia 3:13-14 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ungama dhambi zako tu: kwamba umemwasi BWANA Mungu wako, umetapanya wema wako kwa miungu ya kigeni chini ya kila mti unaotanda, nawe hukunitii mimi,’ ” asema BWANA. “Rudini, enyi watu msio waaminifu, kwa kuwa mimi ni mume wenu,” asema BWANA. “Nitawachagua ninyi, mmoja kutoka kwenye mji, na wawili kutoka kwenye ukoo, nami nitawaleta Sayuni.